27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

NBC Tanzania Open Championship 2021 kuunguruma Des 3-5 Lugalo

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

MASHINDANO ya gofu ya NBC Tanzania Open Championship 2021 yanatarajia kuanza Desemba 3-5, mwaka huu kwenye viwanja ya Klabu ya Gofu Lugalo, jijini Dar es Salaam.

Michuano hiyo mikubwa ya kufunga mwaka ya kalenda ya Chama Cha Gofu Tanzania (TGU), itashirikisha wachezaji wa mataraja tofauti ambao ni wa kulipwa, ridhaa vijana na wazee.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Novemba 29,2021 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Klabu ya Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwongo, amesema washiriki wa miachuano hiyo wanatarajiwa kufika zaidi ya 100 kutoka klabu zote za Tanzania.

Amesema mashindano hayo yanaratibiwa na TGU lakini Lugalo imepewa heshima ya kuyaendesha.

“TPDF Lugalo Golf Club, imeandaa shindano kubwa sana, naweza kusema ni shindano kubwa kuliko yote ambalo linafahamika kama NBC Tanzania Open Golf Championship 202.

Makamu Mwenyekiti wa TGU, Kanali David Luoga, akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) leo Novemba 29,2021, Lugalo jijini Dar es Salaam.

“Hili ni shindano kubwa kwa maana limeratibiwa na TGU ambayo ndio chama chetu kikuu cha gofu hapa nchini wametupa hiyo heshima.

“Sisi kama klabu tumejiandaa kasi ya usajili ni kubwa, pia tumefanya marekebisho ya viwanja na kutakuwa na wasaidizi uwanjani tumeshawaandaa tayari,” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Wateja Binafsi na Wafanyabiashara ndogondogo wa benki ya NBC ambao ndiyo wadhamini wa michuano hiyo, Elibariki Masuke, amesema ni mara ya kwanza kudhamini gofu na wanatarajia kuendelea kusapoti mchezo huo.

Masuke amesema amshindano hayo ni muhimu kwa sababu yanahisisha watu mbalimbali na ndiko vinakotoka vipaji vya gofu, watahakikisha wanaunga mkono jitihata za Jeshi za kukuza michezo.

“Mashindano haya yanahusisha watu wengi, lakini pia wateja wa NBC ambao kwetu sisi ni watu muhimu sana.Huu ni mwanzo tu, napenda kuwahakikishia wadau wa michezo kuwa NBC itaendelea kuwa mstari wa mbele kuhakikisha mchezo wa gofu unakuwa nchini,” ameeleza Masuke.

Naye Makamu Mwenyekiti wa TGU, Kanali David Luoga, ameishukuru NBC kwa udhamini huo na wadau wote wa gofu kwa sababu hayo ni mashindano ya mwisho kwa mwaka huu kwa mujibu wa kalenda yao.

Kanali Luoga amesema wachezaji wa daraja A watacheza mashimo 72 kuanzia Des 3-5,daraja B, wazee na wanawake watacheza mashimo 36 kuanzia Des 4-5.

Klabu zitazoshiriki michuano hiyo ni Moshi Klabu, Arusha Gymkhana,Dar es Salaam Gymkhana, Sea Cliff Klabu Zanzibar, Kill Golf Klabu na TPC.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles