23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, October 16, 2021

Messi amnyima mtu jezi


BAADA ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) jana, beki wa Reims, Andrew Gravillon, alimfuata staa wa PSG, Lionel Messi, ili ampe jezi lakini Muargentina huyo alikataa.


Mbele ya mashabiki 20,000, ambapo PSG walishinda mabao 2-0, Messi alitokea benchi na hakufunga katika mechi yake hiyo ya kwanza tangu aliposajiliwa.


“Nilimfuata anipe jezi ili nimpelekee mdogo wangu lakini hakunipa. Labda nitabahatika siku nyingine,” amesema Gravillon.
Messi anatarajiwa kushuka tena mzigoni Septemba 12, mwaka huu, siku PSG watakapokuwa nyumbani kukipiga na Clermont Foot katika mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
161,801FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles