23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 27, 2023

Contact us: [email protected]

Guardiola: Arteta bonge la kocha

KWA mujibu wa Pep Guardiola, mashabiki wa Arsenal wasiwe na hofu juu ya uwezo wa Mikel Arteta kwani ndiye aliyekuwa siri ya mafanikio ya Manchester City akiwa msaidizi wake.


Guardiola anaibuka na utetezi huo wakati mashabiki wa Arsenal wakiwa hawataki hata kumsikia Arteta baada ya timu yao kupoteza mechi zote tatu za msimu huu wa Ligi Kuu ya England.


“Sizungumzi hivi kwa kuwa ni rafiki yangu, nazungumza kiweledi. Nilipokuwa naye, alinifundisha mambo mengi, ambayo yalisaidia katika yale tuliyofanikiwa,” amesema Guardiola.
Wakati jina la Arteta likihusishwa na mlango wa kutokea pale Emirates, kocha aliyewahi kufungashiwa virago Chelsea, Antonio Conte, ndiye anayetajwa kurithi mikoba yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,729FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles