Erick Mugisha -Dar Es Salaam
Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya wanawake wa kislam (HASSANAYN) ambayo inashughulika na kuhudumia kwa watoto yatima, watoto wanaishi kwenye mazingira magumu, wazee na shughuri nyingine za kijamii wamepokea msaada wa vifaa vya kukarabatia ofisi kutoka kwa mdau wa maendeleo hapa nchini.
Akizungumza na MTANZANIA leo Mdau wa Maendeleo, Mwantumu Mgonja alisema taasisi ya wanawake wa kislamu imefanya jambo zuri kwa kufungua kikundi hicho kwa ajiri ya jamii maana watoto wengi wamekuwa wakikosa malezi bora na huduma za kifamili kutokana na hali ya kiuchumi.
“Napongeza sana taasisi hiyo kwa kutoa huduma hizi maana watoto wengi wamekuwa wakijiingiza kwenye makundi mabaya ya wizi, ujambazi, utumiaji wa madawa ya kulevya hivyo nitashirikiana bega kwa bega kadri ya uwezo wangu.
“Pia nimeamua kutoa vifaa hivyo vya kukarabatia ofisi kwa kuonesha mwanga kwa watu binafsi na Taasisi watakao guswa na ilikuweza kuwasaidia watoto yatima, wasiojiweza na wazee maana wote ni wamoja bila kuangalia dini wala ukabila”, alisema Mdau wa Maendeleo, Mgonja.
Katibu wa (HASSANAYN), Mayasa Shomvu alisema kabla ya kufunguliwa kwa taasisi hiyo kulikuwapo na darasa la kutoa elimu ya kidini kwa wanawake na kusaidia watoto yatima, wasiojiweza, wazee na shughuri nyingine za kijamii ndipo tukaamua kuwanzisha taasisi hiyo ilikuwasaidia kwa upana zaidi.
Alisema taasisi hiyo inatoa huduma zake bila kuangalia dini wala kabila na tumeshafanya usajili wa taasisi yetu kwa kufata masharti kwa kupitia serikali za mitaa hadi halmashauri ya wilaya ilikutaka kutoa huduma vizuri na hata akitokea muwezeshaji anaweza kuitambua taasisi hiyo.
“Tulianza kwa kutunga katiba na kanuni kwa kuchagua viongozi katika taasisi yetu pia kulifata taratibu za kufanya usajili kwa pita njia zote za kisheria kuanzia bakwata hadi serikalini kwa kufanya kazi ya kutoa huduma kwa kutambulika kisheria.
“Pia tunamshukuru mdau wetu, Mwantumu Mgonja kwa kutuletea vifaa vya kukarabati ofisi maana ilikuwa changamoto kubwa sana katika ufanyaji kazi pia tunaomba watu kujitokeza iwe mtu binafsi au Taasisi kujitokeza katika utoaji wa misaada kwa chochote kile ilikuweza kuwasaidia wanajamii”, alisema Katibu Shomvu.