27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Ummy Mwalimu: Epukeni safari za nje zisizo za lazima

Aveline Kitomary

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka Watanzania kuepuka safari za nje zisizo za lazima hasa katika maeneo yaliyoathirika na virusi vya corona na badala yake wafanye biashara za mtandaoni.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Jumamosi Februari 29, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa hadi sasa hakuna mtu mwenye virusi hivyo kwa Tanzania.

“Tangu Januari 30, Serikali ilivyotangaza kuwa corona ni janga la kimataifa  tumechunguza  watu 1,148 katika mipaka hasa wale wanaotoka katika nchi zilizoathirika ikiwemo china tunafanya uchunguzi kutumia vipimo na tunavipima joto 140.

“Tumeongeza idadi ya wataalmu wa afya sasa wako 100 ili kuimarisha ufuatiliaji wa wasafiri, tumeandaa dawa, vifaa kinga na vitakasa mikono ziko bohari ya dawa na tumetenga maeneo maalumu na tuna uwezo wa kupima virusi hivyo ndani ya saa nne hadi sita kupitia NIMR,” amesema Waziri Ummy.

Ameongeza kuwa amewasiliana na ubalozi wa china nchini Tanzania na kwamba wanafunzi 504 walioko nchini China hali zao ni nzuri.

Idadi ya wagonjwa imeendelea kuongezeka kwani hadi February 27 watu 83,652 wamethibitika kuugua huku 2,858 wamefariki dunia, asilimia 94 ni kutoka nchini China.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles