32.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge aeleza baba aliyembaka, kumlawiti mtoto wake alivyokutwa na hatia akaachiwa

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Adelardus Kilangi, amesema ofisi yake inafuatilia sakata la mtoto wa miaka 11 anayedaiwa kubakwa na baba yake mzazi, Aristerico  Silayo ambaye licha ya kubainika ana makosa aliachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Amesema ikibainika kuna mawakili na wanasheria walikula njama kwenye tukio hilo na kukiuka maadili ya kazi, watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria kwa kupelekwa kwenye kamati za maadili zilizopo chini ya mahakama.

Prof Kilangi alitoa kauli hiyo jana wakati akijibu hoja mbalimbali za waliochangia katika mjadala wa muswada sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali namba 3 wa mwaka 2019.

Kauli hiyo inatokana na mwongozo wa Mbunge wa Viti Maalum, Amina Mollel (CCM) ambaye alihoji kuhusu uamuzi wa Mahakama kumwachia huru baba aliyembaka mwanae mkoani Arusha.

Molel alisema licha ya mtuhumiwa huyo, kukutwa na hatia mtoto huyo amekosa haki katika Mahakama ya Arusha hivyo mtuhumiwakuachiwa huru.

Katika taarifa yake Amina alisema watoto ni maua na baraka kutoka kwa Mungu na kwamba mahakama ndio chombo cha kupata haki kwa kila mwananchi.

Alisema kuwa inasikitisha sana pale ambapo haki hasa kwa wanyonge inapodhulumiwa na kupokonywa na vyombo vilivyopewa dhamana.

“Nina masikitiko makubwa nikiwa kama mama, mwanamke ninasimama kwa ajili ya kusimamia haki ya mtoto ambae amekosa haki katika mahakama ya Arusha,”.

Alisema kuwa mtoto huyo kwa muda mrefu alikuwa akibakwa na baba yake mzazi kwa kuingiliwa mbele na nyuma hivyo kuharibika kwa kiasi kikubwa.

 “Lakini mheshimiwa Naibu Spika jambo la kusikitisha ni kwamba yule mtoto amekosa haki, baba mzazi ameshinda.. Baadhi ya mawakili waliokuwa wakitetea haki hii.

“Ninaomba kwa sababu leo wanasheria wapo hapa, Waziri wa Katiba na Sheria, Mwanasheria Mkuu wa Serikali baadhi ya matamshi yaliyokuwa yakitolewa na hoja ya wawakili ni ndugu huyu baba aliyembaka mtoto sasa kesi ya nyani tunawezaje kuipeleka kwa tumbili haiwezekani,”alisema.

Alisema moja ya majibu waliyokuwa wakipata ni kwamba moja wa mawakili alimwambia mwalimu ambaye amesimamia hilo suala mpaka kuhakikisha linaletwa bungeni kuonana na wabunge.

“Wakili anamwambia wewe mwalimu naomi wewe unasimamia hii kesi unajidai king’ang’anizi mbona watu ambao wameingiliwa mpaka na mbwa wanafanya mapenzi nao na hakuna lolote linalofanyika,”alisema.

Alihoji, kama wanasheria wamefikia mahali hapo pasipo kusimamia kesi ya haki ya huyu mtoto taifa hili tunalienda  wapi.

Molel alinukuu barua inayohusu hukumu ya shauri la jinai la mtoto wa miaka 11 shauri namba 339/2017 mahakama ya mkazi Arusha ambayo inatoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwenda kwa AG ambayo iliandikwa Januari 9 mwaka huu.

Kupitia barua hiyo, Amina alisema shauri hilo lilisikilizwa kwenye mahakama ya Mkazi Mkoa wa Arusha, na kutolewa hukumu Desemba 14 mwaka 2018.

Ilieleza kuwa katika shauri hilo mtuhumiwa alikuwa na hatia na mahakama dhidi ya ubakaji.

Kupitia barua hiyo, alisema  kwa kutumia kifungu cha 235 cha sheria ya makosa ya jinai Hakimu Mwankunga aliwachia huru mtuhumiwa 

Ofisi hii inashauri ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuipatia kwa makini hukumu hiyo ili jamhuri iweze kukata rufaa ndani ya siku 45

Alisema kwenye shauri hiyo rufaa haijakatwa kwakuwa mtuhumiwa anatishia watu hivyo hakuna anayeweza kwenda mahakamani.

Akijibu sakata hilo Dk. Kilangi alisema ”Ofisi yangu itafuatulia suala hilo na kama itabainika kuna mahakimu wamekiuka maadili ya kazi watachukuliwa hatua.”

“Iwapo itagundulika kuwa hakimu aliyehusika kutoa hukumu hakufuata maadili ya kazi yake zipo kamati za maadili chini ya mahakama na vyombo vingine. Wanasheria waliohusika ipo kamati ya nidhamu ya mawakili hivyo wakigundulika watafikishwa huko hivyo naahidi tutalifuatilia suala hilo,”alisema.

Awali akijibu mwongozo huo, Naibu Spika alitoa rai kwa wanaume kuacha watoto wakue kwakuwa wanawake  mtaani wako wengi na wakutosha.

“Na huyu babaa kama ni kweli kamfanyia mtoto wake lakini hata kama si yeye basi yupo mtu mwingine ambaye amemfanyia mtoto huyu vitendo kama hivyo..

“Vitendo kama hivi vinaumiza na huyu mtoto hawezi kukua katika hali ya kawaida kama watoto wengine lakini sisi kama wawakilishi waheshimiwa wabunge na sisi tuwe mfano bora kwa jamii,”alisema

 “Umezungumzia siku 45 hivyo zisikutishe maana utaratibu upo hata kama siku zimepita bado anaweza kuchukuliwa hatua kwakuwa utaratibu wa kuomba rufaa nje ya ya wakati na mahakama zinatoa ruhusa hiyo,”alisema.

“Kwa taratibu za kisheria kama kesi imeamriwa na hakimu mkazi kuna ngazi nyingine za kukata rufaa na kwamba huo ndio utaratibu wa kawaida hivyo kama ingekuwa imeamriwa na mahakama ya rufani pale ndio mwisho inabidi ufuate taratibu nyingine za kuitaka mahakama hiyo iangalie upya hukumu uliyotolewa.

“Lakini kwakuwa hukumu imetolewa na hakimu mkazi utaratibu wa kisheria upo wa kukata rufaa.. pamoja na hayo niseme nami naungana na mheshimiwa Amina kwa uhalisia wa jambo hilo kwamba kuna mtoto ambaye amefanyiwa vitendo vya ukatili.

“Sasa kwa sababu kama ninavyosema sina namna ya kusema ni baba aliyefanya ama mtu yeyote Yule lakini kimsingi ni kwamba haya si mambo mazuri kutokea katika jamii yetu,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles