27 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Matic: United hii ubingwa tusahau

MANCHESTER, ENGLAND

KIUNGO wa Manchester United, Nemanja Matic, ameweka wazi kuwa, wana wachezaji wazuri vijana, lakini kutokana na kukosa uzoefu ubingwa wa Ligi Kuu msimu ujao watausikia kwa wengine.

Mchezaji huyo anaamini kikosi hicho cha kocha Ole Gunnar Solskjaer, kinahitaji wachezaji wenye uzoefi mkubwa ili kuleta ushindani katika mbio za kuwania ubingwa.

Matic mwenye umri wa miaka 30, anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wenye nafasi kubwa ya kupewa unahodha katika msimu mpya wa ligi. Katika michezo ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya mchezaji huyo amecheza michezo yote ya ushindi dhidi ya Perth Glory, Leeds, Inter Milan na Tottenham.

“Wachezaji bora na wenye uzoefu wanaweza kukupa taji, kwenye kikosi chetu tuna wachezaji wengi wazuri, lakini hawana uzoefu.

“Tuna wachezaji watano au sita wenye uwezo mkubwa, ila bado ni vijana kama vile Marcus Rashford na Anthony Martial. Wamekuwa kwenye kiwango cha hali ya juu, lakini bado hawana mchango wa kuweza kuipa timu ubingwa.

“Mason Greenwood ni faida ya baadae, najua Man United wapo kwenye mipango ya baadae kwa wachezaji waliowasajili, lakini wanatakiwa kupewa muda kwa kuwa ukiwa na miaka 17 hawezi kufanya kama mtu mwenye umri wa miaka 26 au 27.

“Siku zote soka linahitaji matokeo, lakini mashabiki wanatakiwa kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki ninaamini kwa wachezaji waliopo wanaweza kuifanya Man United kurudi kwenye heshima yake hapo baadae,” alisema mchezaji huyo.

Kiungo huyo mkabaji raia wa nchini Serbia, ana uzoefu mkubwa na Ligi ya England, alikuwa miongoni mwa wachezaji waliochukua Ligi Kuu England mwaka 2015 na 2017 katika kikosi cha Chelsea kabla ya kujiunga na Man United.

Ligi Kuu England inatarajiwa kuanza Agosti 9 mwaka huu huku Manchester United wakishuka dimbani Agosti 11 dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wao wa ufunguzi ambao utapigwa kwenye uwanja wa Old Trafford.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles