28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mashabiki wamjia juu Wenger

hi-res-355d44df889713435191347cbb30cf12_crop_exactLONDON, ENGLAND

BAADA ya klabu ya Arsenal kutolewa katika michuano ya Kombe la FA juzi dhidi ya Watford, mashabiki wa klabu hiyo ya jijini London wamemjia juu kocha, Arsene Wenger na kumtaka aondoke.

Arsenal walikuwa mabingwa watetezi wa kombe hilo, lakini wameshindwa kulitetea na kukubali kichapo hicho cha mabao 2-1 na kuwafanya mashabiki kumtaka Wenger afungashe virago vyake.

Mashabiki hao wamemshambulia kocha huyo kupitia mitandao ya kijamii, lakini amewataka kuwa wavumilivu na kuiunga mkono timu yao hasa katika michezo ijayo.

“Arsenal imepoteza michezo mingi na imetolewa kwenye michuano ya Kombe la FA, mashabiki wanatakiwa kuvumilia na kuangalia michezo ijayo ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa.

“Hii ni timu yao wanatakiwa kukubaliana na chochote kinachotokea sio siku zote tutakuwa na furaha, kuna wakati mambo yanakuwa magumu lakini tunatakiwa kuwa pamoja katika kila mchezo, najua inauma sana hasa unapopoteza mchezo ukiwa nyumbani ila ndivyo soka lilivyo,” alisema Wenger.

Wenger anaamini nguvu zake anazielekeza katika michuano ya Ligi Kuu nchini England na Ligi ya Mabingwa, ambapo kesho klabu hiyo itashuka dimbani kupambana na mabingwa Barcelona kwenye Uwanja wa Nou Camp, huku mchezo wa awali Arsenal wakiwa nyumbani walikubali kichapo cha mabao 2-0.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles