23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Shabiki Dortmund afia uwanjani

DORTMUND, UJERUMANI

SHABIKI wa klabu ya Borussia Dortmund, amefariki dunia juzi wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mainz 05, kwenye Uwanja wa Signal Park.

Katika mchezo huo, Dortmund ilifanikiwa kushinda mabao 2-0 ambayo yalifungwa na Marco Reus pamoja na mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Manchester United, Shinji Kagawa, lakini hakushangilia kutokana na kifo cha shabiki huyo.

Shabiki huyo alipoteza maisha katika dakika ya 30 ya mchezo huo baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo.

Taarifa ya kifo cha shabiki huyo zilienea ndani ya dakika 15 ambapo idadi kubwa ya mashabiki walipata taarifa hadi kufikia wakati wa mapumziko. Kipindi cha pili kilipoanza wachezaji wote pamoja na mashabiki walisimama kwa ajili ya kufanya maombi ya kifo hicho.

Hata hivyo, shabiki mwingine alikimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu baada ya kupoteza fahamu kutokana na mshtuko wa moyo, lakini hali yake inadaiwa kuendelea vizuri.

Rais wa klabu ya Dortmund, Reinhard Rauball, kupitia mtandao wa klabu hiyo ametuma salamu za pole kwa familia ya marehemu na mashabiki wote kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles