27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Man City kumalizana na Dynamo Kyiv leo

Dynamo-Kiev-vs-Manchester-City-702x336-1050x600MANCHESTER, ENGLAND

MASHABIKI wa klabu ya Manchester City leo wanasubiri kwa hamu kuiona timu yao ikiingia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Leo klabu hiyo itakuwa kwenye Uwanja wa Etihad na kuwakaribisha wapinzani wao Daynamo Kyiv, huku City ikiwa na uhakika wa kusonga mbele.

Kutokana na ubora wa Man City ni wazi kwamba ina kazi ndogo sana leo hii kutokana na ubora wao na timu ambayo wanakutana nayo huku wakiwa nyumbani.

Mchezo wa awali City ilifanikiwa kutoa kichapo kwa Dynamo Kyiv cha mabao 3-1, hivyo katika mchezo wa leo wanahitaji ushindi au sare ya aina yoyote kuweza kusonga mbele, wakati huo Dynamo wakihitaji ushindi wa mabao 3-0, ambapo ni wazi kwamba kazi ni ngumu kwao.

Mchezo mwingine ambao utapigwa leo ni kati ya Atletico Madrid ambao watakuwa nyumbani na kuwakaribisha PSV.

Huu ni mchezo ambao unaonekana kuwa mgumu sana kutokana na ubora wa timu zote na ukiangalia katika mchezo wa awali uliopigwa Uholanzi huku PSV walikuwa wenyeji mambo yalikuwa magumu hakuna timu ambayo ilishinda.

Katika mchezo huu wa kesho chochote kinaweza kutokea na kila mmoja anasubiri kosa la mwenzake ili aweze kutumia nafasi, huu ni mchezo ambao makocha wa pande zote mbili kuonesha ufundi wake kuweza kupata bao la mapema na kuweka ulinzi, hata hivyo inawezekana katika mchezo huu mabao yakawa machache sana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles