25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mashabiki Everton wamtimua Iwobi

MERSEYSIDE, England

MASHABIKI wa Everton wanataka kiungo raia wa Nigeria, Alex Iwobi, aondoke klabuni hapo baada ya kiwango kibovu katika kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Manchester City.

Iwobi aliyetua Everton mwaka juzi akitokea Arsenal, alitokea benchi dakika ya 17 kuchukua nafasi ya majeruhi Demarai Gray lakini alicheza kwa kiwango kibovu, ikiwamo kupoteza pasi na kumaliza mchezo bila kupiga hata shuti moja.

Huo ni mwendelezo wa majanga kwa Iwobi kwani amefunga mabao matatu pekee katika mechi 65 tangu aliposajiliwa na wapinzani hao wa Liverpool.

Katika mtandao wa Twitter, mmoja ya mashabiki hao alisema klabu nyingi zinaingia chaka kumsajili nyota huyo zikidhani ana uwezo kwa kuwa mjomba wake ni Jay Jay Okocha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles