23.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Mchumba wa Khashoggi amwangukia Bieber

LOS ANGELES, Marekani

MCHUMBA wa aliyekuwa mwandishi wa habari maarufu wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi, amemwandikia barua staa wa muziki wa Pop, Justin Bieber, akimwomba kutokwenda kufanya ‘shoo’ katika taifa hilo la Kiarabu.

Bieber anatarajiwa kuingia Saudi mwezi ujao lakini bibiye Hatice Cengiz amemtaka kubadili uamuzi ili uwe ni ujumbe dhidi ya Serikali ya nchi hiyo iliyohusika katika kifo cha mpenzi wake, Khashoggi.

Khashoggi aliuawa mwaka 2018 akiwa jijini Istanbul, Uturuki, huku ikielezwa kuwa ulikuwa ni mpango wa Serikali ya Saudi kwa kuwa alikuwa akiikosoa mara kwa mara.

Katika ujumbe wake kwa Bieber, Hatice aliyekwishavishwa pete na Khashoggi, amesema: “Usiende kuwaimbia watu waliohusika kumuua mpenzi wangu, Jamal.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles