21.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mariah Carey aomba kuolewa

Mariah Carey
Mariah Carey

LOS ANGELES, MAREKANI

ALIYEKUWA mke wa msanii, Nick Cannon, Mariah Carey, ambaye kwa sasa amechumbiwa na bilionea kutoka Australia, James Packer, amemtaka mchumba huyo amuoe mapema.

Mariah na Cannon walikuwa katika mgogoro mara baada ya kuachana huku kila mmoja akitaka alee watoto wao wawili, lakini baada ya Mariah kushinda kesi hiyo amemtaka mchumba wake huyo wa sasa amuoe mapema.

“Kesi yangu imekwisha salama, hivyo nipo huru kuwa na familia yangu, lakini kilichobaki kwa sasa ni kuolewa na Packer mara baada ya kumalizika kwa kesi hiyo.

“Mambo yalikuwa yameyumba kutokana na kesi hiyo, lakini nimemwambia Packer afanye mipango ya kunioa mapema iwezekanavyo kwa kuwa hakuna tatizo lolote kwa sasa,” aliandika Mariah.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles