31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani yaishutumu Israel ujenzi wa makazi

obamaWASHINGTON, MAREKANI

SERIKALI ya Marekani imeshutumu vikali hatua ya Israel ya kuidhinisha mipango mipya ya ujenzi wa nyumba katika eneo la Ukingo wa Magharibi.

Ikulu ya Marekani na Wizara ya Masuala ya Kigeni imesema mipango ya kujenga nyumba mpya 300 pamoja na eneo la viwanda inaathiri mpango wa uwapo wa mataifa mawili huru, kufuatia migogoro kati ya Israel na Palestina.

Israel imesisitiza kuwa ni ujenzi wa chini ya nyumba 100 ulioidhinishwa.

Waziri wake wa masuala ya kigeni alisema nyumba mpya zitajengwa katikati ya maeneo ya makazi yaliyopo.

Takribani raia 570,000 wa Israel wanaishi katika zaidi ya nyumba 100 zilizojengwa tangu Israel ikalie maeneo hayo yaliyopo eneo la Ukingo wa Magharibi na Mashariki mwa Yerusalem mwaka 1967.

Makazi hayo yanatajwa kuwa haramu chini ya sheria ya kimataifa, ijapokuwa Israel inapinga hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles