22.7 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Simu ya Samsung yawaka moto ndani ya ndege

galaxyMARYLAND, MAREKANI

SIMU iliyotengenezwa na Kampuni ya Samsung aina ya Galaxy Note 7 na kuthibitishwa kuwa salama, imeshika moto kwenye ndege nchini Marekani.

Simu hiyo inadaiwa kushika moto ikiwa mikononi mwa abiria aliyekuwa kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Southwest.

Shirika hilo limesema abiria waliokuwa kwenye ndege iliyokuwa imepangwa kusafiri kutoka Louisville, Kentucky, hadi Baltimore, Maryland, waliondolewa kwa dharura kabla ya ndege hiyo kuruka juzi Jumatano.

Kampuni ya Samsung imewashauri watu waliokuwa wamenunua simu za Note 7 kuzirejesha walikozinunua ili zirudishwe kiwandani, baada ya kugunduliwa zilikuwa na tatizo kwenye betri zake.

Samsung imesema bado inachunguza  ili kuthibitisha chanzo cha moto huo.

“Tunashirikiana na maofisa wa Serikali na wa Shirika la Ndege la Southwest kupata simu hiyo na kuthibitisha chanzo cha moto huo,” ilisema kampuni hiyo kupitia taarifa yake.

Msemaji mmoja wa shirika hilo alisema: “Abiria mmoja alitufahamisha kuhusu moto uliokuwa unafuka kutoka kwenye simu. Abiria wote na wahudumu wa ndege waliondolewa salama kutoka kwenye ndege hiyo.”

Mmiliki wa simu hiyo, Brian Green, akizungumza na Jordan Golson wa Shirika la The Verge, alisema alinunua simu hiyo Septemba 21, mwaka huu.

Alisema simu hiyo ilikuwa na alama ya mraba wa rangi nyeusi kwenye kasha lake ili kutofautisha kati ya simu zilizokuwa zimeuzwa awali zilizodaiwa kutokuwa salama na zile mpya zilizochunguzwa na kupitishwa kuwa ni salama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,580FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles