25 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 6, 2022

Contact us: [email protected]

Luna aomba radhi kusambaa kwa mkanda wake wa ngono

maxresdefaultEIBAR, HISPANIA

NYOTA wa zamani wa klabu ya Aston Villa, Antonio Luna, ameomba radhi kwa mashabiki wake kutokana na kuenea kwa video yake ya ngono ambayo alicheza na mchezaji mwenzake, Sergi Enrich wa klabu ya Eibar ya nchini Hispania.

Wawili hao kwa sasa wanakipiga katika klabu hiyo ya Sergi Enrich, lakini kwa sasa wamekutwa na kashfa ya kuenea kwa video yao ya ngono ambayo wameicheza wawili hao.

Hata hivyo, kuna video ambayo inasambaa kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha Luna akimuomba radhi mchezaji mwenzake huyo Enrich.

Luna aliwahi kuwa mchezaji wa Sevilla kabla ya kujiunga na Aston Villa mwaka 2013 kwa kitita cha pauni milioni 2 na kufanikiwa kucheza michezo 18 kwa kipindi chake hadi 2014. Lakini msimu uliopita alijiunga na klabu ya Eibar ya nchini Hispania.

Hata hivyo, kwa sasa wachezaji hao wote wanaomba radhi kutokana na kitendo hicho ambacho kinazungumziwa kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii.

“Ni kweli kwamba kosa kubwa ambalo tumelifanya kwa video yetu kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na hatuwezi kukataa jambo hilo.

“Wote tunajua kwamba video hiyo inasambaa na tukiwa kama wachezaji wakubwa na wakulipwa tunakiri kuwa tumefanya kosa kubwa sana kwa kuwa wapo wachezaji ambao walikuwa wanafanya mambo kutokana na vile ambavyo tulikuwa tunavifanya.

“Tumejiharibia kwa kiasi kikubwa kila kona kwa sasa na kama tulikuwa kioo kwa jamii ni kweli kwamba kioo hicho kwa sasa kimevunjika, kutokana na hali hiyo tumeona bora tutumie nafasi hii kwa ajili ya kuomba radhi.

“Kwa upande wa klabu ya Eibar tunaamini kulikuwa na kizazi ambacho kilikuwa kinapenda kuona vitu ambavyo tulikuwa tunavifanya, lakini kwa sasa wengi watatuchukia sana.

“Tunaomba radhi kwa jambo hilo, hatujui imekuwaje hadi mkanda huu umesambaa kwenye mitandao ya kijamii, hapa tulipo tuna mawazo mengi sana juu ya jambo hili, tunaomba radhi kwa klabu ya Eibar pamoja na mashabiki wote,” alisema Luna.

Luna alikuwa wa kwanza kufunga bao katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi katika msimu wa mwaka 2013/2014, huku Aston Villa ikishinda mabao 3-1 dhidi ya Arsenal kwenye uwanja wa Emirates.

Mchezaji huyo aliwahi kutumikia klabu ya Sevilla, akajiunga na klabu ya Aston Villa mwaka 2013, huku 2014 alijiunga na Verona kwa mkopo kabla ya kujiunga na Spezia Calcio mwaka 2015 na baada ya hapo alijiunga na Eibar baada ya kuvunja mkataba wake na Aston Villa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,606FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles