WASHINGTON, Marekani
OFISA wa ngazi ya juu wa intelijensia nchini hapa amesema huenda Urusi inakiuka mkataba wa nyuklia kwa kufanya majaribio ya silaha zisizo na nguvu kubwa katika ene la Actic.
Akizugumza mjini hapa jana, Luteni Jenerali Robert Ashley ambaye ni mkurugenzi wa taasisi ya intelijensia amesema serikali ya Urusi pengine inakiuka sheria za mkataba wa pamoja wa CTBT unaozuia majaribio ya nyuklia ambao Urusi ilitia saini mwaka 2008 na ambao Marekani imetia saini lakini haijaanza kuutekeleza.
”Kwa uelewa wetu uendelezwaji wa silaha za nyuklia unatusababisha tuamini kuwa shughuli za majaribio ya Urusi zitasaidia kuboresha uwezo wa silaha za nyukilia,” alisema Luteni Jenerali Ashley.
Ameongeza kuwa Marekani ilitegemea Urusi, ambayo amesema ilikuwa inategemewa kujaribu silaha zake katika visiwa vya Zemlya kuongeza ubora wa silaha za nyuklia kwa muongo mmoja ujao.
Hata hivyo wachambuzi wa mambo wamepokea taarifa hiyo lakini haikuwashawishi.
Shirika linalosimamia utekelezaji wa makubaliano ya mkataba wa nyukilia CTBTO, limesema kwenye taarifa yake kuwa haishuku shughuli zozote zinazokwenda kinyume na mkataba.
CTBT unapiga marufuku majaribio ya silaha za nyukilia popote duniani uliofikiwa kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 1996.