27.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Marcelo kuipa kisogo Madrid

MADRID, Hispania

BEKI wa pembeni wa Real Madrid, Marcelo, amemwambia Rais wa klabu hiyo, Florentino Perez, kwamba ataondoka Bernabeu akiwa mchezaji huru wakati wa usajili wa kiangazi, mwakani.

Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 33, alitua Madrid mwaka 2007 akitokea Fluminense ya Brazil na hadi sasa ameshacheza mechi 530 na kutwaa mataji matano ya La Liga na manne ya Ligi ya Mabingwa.

Marcelo amekuwa akisumbuliwa na majeraha kwa misimu kadhaa sasa na amepoteza nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha vigogo hao wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga).

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, nyota huyo anataka kurejea Fluminense ambako ndiko kipaji chake kilikoibuliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles