30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

United yampa rekodi Jurgen Klopp

MERSEYSIDE, England

BAADA ya kuibamiza Manchester United mabao 5-0, Jurgen Klopp amekuwa kocha wa kwanza kushinda mechi 200 ndani ya muda mfupi.

Katika mchezo huo uliochezwa Old Trafford jana, Liverpool ilikusanya pointi tatu kwa mabao ya Naby Keita, Diogo Jota na Mohamed Salah aliyeingia kambani mara tatu (hat-trick).

Huo ulikuwa ni ushindi wa 200 kwa Klopp katika mechi 331 pekee alizoiongoza timu hiyo tangu aajiriwe mwaka 2015 akitokea Bundesliga alikokuwa akiinoa Borussia Dortmund.

Aidha, Mjerumani huyo amekuwa kocha wa kwanza katika historia ya Liverpool kucheza mechi saba mfululizo bila kufungwa na Manchester United.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles