25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Man City v Arsenal ni Guardiola au Arteta?

KESHO, Manchester City watakuwa kwenye Uwanja wao wa nyumbani (Etihad) kuwakaribisha Washika Bunduki wa Kaskazini mwa Jiji la London, Arsenal.

Ni moja kati ya mechi za kusisimua wikiendi hii, kila timu ikicheza raundi ya tatu tangu msimu huu wa Ligi Kuu ya England (EPL) uanze.

Man City walifungua pazia la msimu kwa kutandikwa bao 1-0 na Tottenham, kisha wakaibuka na ushindi mnono wa mabao Norwich City.

Kwa upande wao, Arsenal chini ya kocha Mikel Arteta walitupa vibaya karata yao ya kwanza kwa kufungwa mabao 2-0 na Brentford iliyopanda daraja.

Je, ni takwimu zipi zinazoufanya mchezo huo wa Jumamosi uwe wa kukata na shoka kwa pande zote mbili? Makala fupi haya yanachambua…

01. Man City hawajafungwa katika mechi 11 za Ligi Kuu walizokutana na Washika Bunduki tangu mwaka 2015. Katika idadi hiyo ya michezo, Man City wameshinda tisa na kutoa sare mbili.

02. Katika mechi saba za Ligi Kuu za hivi karibuni, ni mara moja tu imetokea kwa Arsenal kutikisa nyavu za Man City.

03. Man City waingie uwanjani wakifahamu kuwa Arsenal haijawahi kupoteza mechi zote tatu za mwanzoni mwa msimu wa EPL tangu mwaka 1954-55.

04. Man City haijawahi kupoteza mechi mbili za mwanzoni mwa msimu tangu ilipofanya hivyo msimu wa 2004-05.

05. Kwa mabeki wa Man City, tishio zaidi kwao ni Nicolas Pepe kwani winga huyo ameifungia Arsenal mabao manne katika mechi tano za Ligi Kuu alizocheza hivi karibuni.

06. Hii itakuwa mechi ya 100 ya EPL kwa kipa Bernd Leno tangu ajiunge na Arsenal akitokea Bayer Leverkusen mwaka 2018.

07. Raheem Sterling ni mwiba zaidi kwa Arsenal kwani ‘amewatungua’ ma razote nne alizokutana nao hivi karibuni.

08. Endapo Man City watafunga kwa penalti, basi wataandika historia EPL kwani litakuwa bao lao la 100 kulipata kwa staili hiyo.

09. Endapo Arsenal watachezea kichapo, itakuwa mechi ya tisa mfululizo kufungwa na Man City kwenye ligi. Hiyo itaifanya Arsenal kuwa timu pekee katika historia ya EPL kufungwa mara nyingi na mpinzani mmoja.

10. Katika mchezo wa mwisho wa EPL, Arsenal walimiliki mpira kwa asilimia 35 mbele ya Chelsea. Man City walimiliki asilimia 67 wakicheza na Norwich City.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles