26 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mamilioni ya fedha yatafunwa

MWANDISHI WETU – MOROGORO

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi saba katika halmashauri mbili za Wilaya ya Kilombero na Halmashauri ya Mji wa Ifakara, kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha zaidi ya Sh bilioni 1.3 za makusanyo ya mapato ya ndani.

Mbali na kuwasimamisha kazi watumishi hao, pia Waziri Mkuu ameagiza watumishi hao warejeshe fedha hizo ndani ya siku tatu kabla hajamaliza ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro. 

Watumishi hao ni pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Fransis Ndulane ambaye anadaiwa Sh milioni tano alizoingiziwa katika akaunti yake bila maelezo yeyote.

Waziri Mkuu amewasimamisha kazi watumishi hao jana  wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, akiwa katika siku ya pili za ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.

 “Mkoa mzima wa Morogoro umekuwa na tatizo la upotevu wa mapato, fedha zinakusanywa zinapita mikononi mwa watu hazifiki benki, hii ni shida, hatutavumilia,” alisema Majaliwa 

Alisema kwa mujibu wa taarifa ya Mkaguzi wa Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), katika  kipindi cha mwaka 2016 hadi Juni 2019, katika Mji wa Ifakara  makusanyo yalikuwa Sh bilioni 2.7  ambapo fedha iliyopelekwa benki ni Sh bilioni 1.9 na kwamba kiasi cha  Sh milioni 727 hazijulikani zilipoenda. 

Alisema katika mitambo 10 ya ukusanyaji wa mapato iliyokaguliwa imeonyesha kiasi cha Sh milioni 348 zilizokusanywa hazikupelekwa benki na hivyo kuishia mikononi mwa watu.

 Waziri Mkuu alisema katika uchunguzi huo, ilibainika kuwa fedha hizo ziliingizwa katika akaunti mbalimbali za watumishi wa halmashauri hizo kutoka kwa Mtendaji wa Kata ya Viwanja 60 katika Mji wa Ifakara, aitwaye Gregory Midas.

Watumishi  hao ni  Reina Mrema ambaye anadaiwa kuchukua kiasi cha Sh milioni 298, Haile Njitango Sh  milioni 73 , Linus Mdembo Sh milioni 2 kwa kushirikiana na mtendaji huyo wa kata.

Pamoja na hali hiyo, Majaliwa aliagiza Mkuu wa Kitengo cha Tehama katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara, John Mvanga ambaye ndiye alibaini kuwepo na ubadhilifu wa fedha hizo na baadae kusimamishwa kazi, arejeshwe kazini mara moja na asibugudhiwe.

 “Mlimsimamisha kazi  kwa sababu mlijua amegundua madudu yenu, lakini haisaidii, arejeshwe kazini, naagiza apewe ulinzi wa kutosha,” alisema Majaliwa 

Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Waziri Mkuu  alisema zaidi ya Sh milioni 600 hazijulikani zilipo huku kiasi cha Sh milioni 98.5 zikidaiwa kuingizwa katika akaunti za watumishi wa halmashauri hiyo bila maelezo yeyote.

Waziri Mkuu amewataja watumishi hao kuwa ni David Onyango aliyechukua kiasi cha Sh milioni 51, Elakada Kanongole Sh milioni 36, Fork Karunde Sh milioni 8 na Charlse Chali Sh milioni 2.5.

Alisema kati ya milioni hizo 600 kampuni ya Kilombero Plantation LTD (KPL) ambao wanadaiwa kiasi cha shilingi milioni 531 ambazo hazikuingizwa katika mfumo huo.

Waziri Mkuu yupo katika ziara ya kikazi mkoani Morogoro tangu juzi, ambapo pamoja na mambo mengine aliagiz

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles