Mchambuzi atimuliwa studio kwa kauli ya ubaguzi dhidi ya Lukaku

0
573

MILAN, ITALIA

Kituo cha Televisheni nchini Italia, kimemfukuza kazi mchambuzi wa soka, Luciano Passirani kwa maoni ya ubaguzi wa rangi juu ya straika wa timu ya Inter Milan, Romelu Lukaku ambaye aliwahi kucheza Manchester United.

Passirani akizungumza kwenye kituo cha televisheni kama mchambuzi alitamka  maneno ya kibaguzi dhidi ya straika huyo raia wa Ubelgiji, kwamba huwezi kuchukua mpira mchezaji huyo akiwa anaumiliki na ili uweze kuuchukua ni lazima umrushie ndizi 10 ili aachie mpira huo.

Baada ya kauli hiyo, Passirani (80) aliomba msamaha lakini alikuwa amechelewa kwani mwongozaji wa kipindi hicho, Fabio Ravezzani alichukua hatua ya kumfukuza kazi mchambuzi huyo akiwa studio.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here