33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

MAMBO USIYOYAFAHAMU KUHUSU BILLY GRAHAM


MWANDISHI WETU NA MASHIRIKA |

MWINJILISTI Billy Graham, raia wa Marekani ni mmoja wa wahubiri maarufu katika karne iliyopita amefariki dunia wiki iliyopita nyumbani kwake Carolina Kaskazini, nchini Marekani, akiwa na miaka 99.

Katika taaluma yake iliyodumu zaidi ya miaka 60, anaaminiwa kuwahubiria mamilioni ya watu kwenye mikutano yake.

Maisha yake alijikita kuendesha mikutano ya dini pamoja na kuwa mshauri wa marais mbalimbali akiwamo Barrack Obama, Harry Truman, Dwight D. Eisonhower, Lyndon B. Johnson, Richard Nixon na wengineo.

Kwa upande huo huo Graham pia aliungana na waandamanaji waliokuwa wakipiga vita dhidi ya Vietnam.

Aidha, Graham alikuwa rafiki binafsi wa Malkia Elizabeth II na familia yote ya Kifalme ya Uingereza.

Graham ambaye alizaliwa Novemba 7, 1918, alijiunga na Shule ya Sekondari Sharon na baadaye Chuo cha Bob Jones huko Illinois, kabla ya kwenda Chuo cha Trinity kilichomilikiwa na Taasisi ya Biblia ya Florida.  Mwaka 1940, Graham alijiunga na Chuo cha Wheaton huko Wheaton katika masomo ya Sayansi ya jamii na utamaduni na kuhitimu mwaka 1943. Baada ya kuhitimu alimuoa mwanafunzi mwenzake Ruth McCue Bell, ambaye wazazi wake walikuwa wakiishi nchini China kutoa huduma za Umisionari. Katika ndoa yao walifanikiwa kupata watoto watano na wajukuu 19.

Mwaka 1949 alianza kufahamika. Baada ya kuhitimu Chuo alipoanzia kuonyesha cheche zake za mahubiri. Aliendesha kipindi cha “Decision Hour” kuanzia mwaka 1950 hadi 1954. Na alikuwa akisikilizwa na watu milioni 215 duniani. Alijenga kanisa lake la kwanza mjini Illinois.

Mwaka 1973 alikuwa mmoja wa waanzilishi wa Mfuko wa Dharura Duniani kusaidia watu wenye matatizo au majanga ya dharura yanayotokea sehemu mbalimbali duniani.

Mwaka 2007 alitangaza kuwa yeye na mkewe mara baada ya kufariki wazikwe pembeni mwa maktaba yake ya nyumbani. Hilo lilipingwa na Patricia Cornwell, aliyekuwa mwandishi wa riwaya na rafiki wa familia hiyo. Graham alistaafu uhubiri mwaka 2005.

Mwaka 2010 alipoteza uoni (kuona vizuri) pamoja na kusikia. Katika maisha yake alikuwa akipingana sana na itikadi ya Ukomunisti, pamoja na kuunga mkono vita baridi ya Marekani dhidi ya Urusi.

Billy alikuwa mwanachama wa chama cha siasa cha Democrat, tangu mwaka 1960. Alipinga uteuzi wa John F. Kennedy kugombea urais kwa sababu alikuwa Mkatoliki na mwenye kutii sheria za Papa.

Aidha, alimini kuwa siasa ni jambo la pili muhimu baada ya masuala ya dini. Mwaka 2012 alimuunga mkono Mitt Romney wa chama cha Republican.

Haya ni baadhi ya masuala aliyoyaamini na kusimama nayo kwenye maisha yake.

Wakati wa ubaguzi wa rangi nchini Marekani, Graham alisema kuwa hangeweza kuhubiria watu waliogawanyika miaka ya 1950 na pia alizungumzia suala la kujumuika na watu wengine.

Katika warsha moja iliyofanyika mjini Tennessee mwaka 1953 alivunja mwiko uliowekwa kutenganisha wazungu na watu weusi kwa wale aliokuwa akiwahubiria.

“Ukristo si wa watu weupe na usiruhusu mtu akuambie ni wa watu weupe au weusi,” aliuambia umati nchini Afrika Kusini mwaka 1973.

Aidha, Graham alikuwa rafiki wa karibu wa Martin Luther King Jr, na wakati mmoja alimlipia dhamana alipokamatwa wakati wa maandamano mwaka 1960 nchini Marekani.

Mwaka 1992 Graham alikuwa mwinjilisti wa kwanza wa kigeni kuzuru Taifa la Korea Kaskazini alikutana na kiongozi wa zamani wa nchi hiyi Kim Il-sung. Pia miaka miwili baadaye alitembelea tena.

Familia yake inauhusiano wa karibu na Korea Kaskazini-aliyekuwa mke wa Graham marehemu Ruth, ambaye wazazi wake walikuwa ni wamisionari, alikulia huko Pyongyang, Korea kaskazini katika miaka 1930.

Katika ziara hiyo Graham alizungumza kuhusu imani yake mbele ya watu wa Chuo kikuu, ilifanyika baada ya idhini ya Rais George H.W. Bush.

Ziara hiyo ilisababisha Graham kutajwa na wengine kama mjumbe asiye rasmi wa Marekani kwenda nchi ambazo hazikuwa na uhusiano mzuri na Marekani wakat huo. Mwaka 1984 alifanya ziara ya siku 12 katika Muungano wa Usovieti na hata kukutana na maafsa wa muugano huo.

Sheria hii inajulikana pia kama sheria ya Mike Pence(Makamu wa rais wa Marekani). Sheria hiyo kuhusu kujizuia hisia zozote kwa mwanamke ilibuniwa na Graham na wainjilisti wengine watatu mwaka 1948 na inahusu ushauri wa Mtume Paulo wa Timoteo kwenye kitabu cha Biblia. Hadi sasa inatumiwa na Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence.

“Tulijiahidi na kujizuia hali yoyote ambayo ambayo ni ya kutiliwa shaka. Kutoka siku hiyo, sikusafiri, kukutana au kula peke yangu na mwanamke mwingine asiye mke wangu.” Alisema Graham

Akizungumza jijini Washington siku tatu baada ya shambulizi la Septemba 11, 2001 Graham alisema kuwa alikuwa na wakati mgumu kupata majibu.

“Nimeulizwa mara mia kadhaa ni kwa nini Mungu aliruhusu taabu kama hii. Ningepeda kusema kuwa sina jibu,” alisema, akiongeza kuwa janga hilo lilikuwa ni funzo kwetu kuhusu kumjali mwingine.

Moja ya masuala yanayokumbukwa katika maisha yake Graham ni wakati alifanya urafiki na mkuu wa genge la wahalifu la Los Angeles Mickey Cohen.

Hata hivyo Cohen hakuitia ombi la Graham la kumtaka aokoke lakini aliendelea na urafiki huo kwa miaka mingi akisema mhalifu anaweza kuwa mhubiri ikiwa angechagua kufanya hivyo.

Kwa miongo kadhaa Graham alihusika na masuala ya White House na kuhudumu kama mshauri asiye rasmi kwa marais.

Aliishia kuwa rafiki wa karibu wa marais hasa Lyndon Johnson na Richard Nixon. Mwaka 2011 wakati wa mahojiano na Christianity Toda, Grahama alisema anajutia kujihusisha na masuala ya siasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles