30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

WAMILIKI WA MAJENGO SASA KULIPIA KODI KIELEKTRONIKI

Na Veronica Kazimoto, Dar es Salaam

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imewataka wamiliki wa majengo nchini kulipia kodi ya majengo ya mwaka 2017/18 hadi kufikia Juni 30, mwaka huu kwa njia ya elektroniki ambapo hakuna muda utakaoongezwa baada ya muda huo kupita.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Charles Kichere amesema TRA haioni sababu ya kuongeza muda wa kulipa baada ya Juni 30, baada ya kuwarahisishia wamiliki kulipia kwa njia ya elektroniki badala ya kupanga foleni.

“Wananchi wanaweza kupata ankara ya malipo kwa majengo yaliyosajiliwa kwenye tovuti ya TRA au simu ya mkononi na kufanya malipo katika tawi lolote la Benki ya NMB au CRDB popote nchini au kwa njia ya mitandao ya simu ya M-Pesa, Tigopesa au Halopesa.

“Tunawaomba wananchi wafuatilie matangazo ya namna ya kulipa Kodi ya Majengo kwa njia ya kielektroniki katika mitandao ya kijamii na kwenye vyombo mbalimbali vya habari au wafike katika ofisi za TRA zilizo karibu na maeneo yao nchi nzima wapate utaratibu wa kulipa kodi hiyo kielektroniki,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Kichere amesema Kodi ya Majengo inalipwa kwa mujibu wa Sheria hivyo, ni muhimu wananchi walipe mapema kodi hiyo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza mwishoni ikiwa ni pamoja na msongamano wa watu.

“Natoa wito kwa wananchi kwamba, wasisubiri mpaka mwisho ndio waanze kupanga foleni kwenye ofisi za TRA, wanatakiwa kulipa kuanzia sasa hivi katika ofisi zetu kwa kutumia njia ya kielektroniki, kinyume na hapo itatubidi tutoze faini kwa atakayechelewa kulipa,” amesema Kichere.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles