23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

HAKIMU ALIYEDAIWA KUTISHIWA MAISHA AFARIKI DUNIA


NA MWANDISHI WETU - DAR ES SALAAM   |  

HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Ilala, Dar es Salaam, Juma Kasailo, amefariki dunia jana kutokana na kile kilichotajwa kuwa ni maradhi ya shinikizo la damu.

Enzi za uhai wake, inadaiwa kuwa Kasailo  alikuwa akipatiwa vitisho na watu wasiojulikana, waliokuwa wakituma taarifa katika mitandao ya kijamii wakimlalamikia kudhulumiwa haki zao.

Februari 16, mwaka huu katika mtandao mmoja wa kijamii, mtu mmoja mwenye jina la Mng’oa Kucha, aliandika ujumbe wenye kichwa cha habari: “Tuondoleeni huyu hakimu Ilala kabla hatujachukua sheria mkononi.”

Mtu huyo alianza kuandika kwa kutaja jina la hakimu huyo, akimlalamikia kwa kutoa hukumu kandamizi kwa watu wasio na fedha.

“Anaitwa Juma Hassan, ni hakimu katika Mahakama ya Ilala…, ni mahiri  kwa kutoa hukumu kandamizi kwa wasio na fedha ya kutosha.

“Hata kama unahitaji kumdhulumu mtu nyumba kesi ikahukumiwa na kufika hadi mahakama ya juu, hakimu huyu ana mamlaka ya kugeuza uamuzi huo na kuufanya upya.

“Tumeripoti sehemu mbalimbali tumechoka, sasa huu mwezi wa mwisho yeyote anayemjua salamu hizi zimfikie,” ulisomeka ujumbe huo ambao kwa sasa nao unasambaa katika mitandao ya kijamii.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili kwa simu jana akiwa nyumbani kwa Kasailo eneo la Kibamba, Dar es Salaam, mmoja wa mahakimu wa mahakama hiyo ambaye hakutaka kuandikwa jina lake gazetini, alisema mara ya mwisho kuonana naye ni juzi akiwa ofisini.

“Hapa nipo msibani, jana (juzi) tulikuwa naye ofisini akiwa analalamika anajisikia vibaya, saa tano asubuhi akaondoka,   baadaye tukasikia amefariki dunia,” alisema hakimu huyo.

Alisema hawezi kutoa taarifa zaidi kuhusu kifo na mazishi ya Kasailo kwa kuwa bado hajapata nafasi ya kuongea na wanafamilia hiyo.

Hakimu huyo alisema enzi za uhai wake alikuwa akimsikia mara kadhaa akilalamikia kuwa anaumwa ugonjwa shinikizo la damu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles