28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Mama awachinja watoto wake, naye kujichinja

Na Derick Milton, Simiyu.

MAMA mmoja aliyejulikana kwa jina la Washi Makingo (35), mkazi wa kijiji cha Laago wilayani Maswa, mkoani wa Simiyu anadaiwa kuwaua watoto wake wawili kwa kuwachinja na kisu kisha naye kujichinja hadi kufa.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi leo  Oktoba 22,2021 kwa waandishi wa habari na Kamanda wa Polisi Mkoa ACP Blasius Chatanda, amesema kuwa mama huyo amefanya  tukio hilo  leo majira ya saa 08:30 asubuhi.

Kamanda Chatanda amewataja watoto waliochinjwa na mama huyo kuwa ni Nseya Kisena (7) na Majaba Kisena (1.5) wote wasukuma ambao walikutwa ndani ya nyumba ya mdogo wake Luja Makigo wakiwa wamekufa pamoja na mama yao.

“Uchunguzi wa awali umeonesha kuwa mama huyo ambaye pia ni marehemu ndiye aliyetekeleza tukio hilo la mauaji, kwake na kwa watoto wake kwa kuanza kumchinja mtoto wake mkubwa wa kike yaani Nseya Kisena na kisha kumchinja mtoto wake mdogo wa kiume Majaba Kisena na hatimaye kujichinja yeye mwenyewe hadi kufa,” amesema Chatanda.

Kamanda huyo ameeleza kuwa mama huyo kabla ya kutenda unyama huo, aliwachukua watoto wake kisha kwenda nao kwa ndugu yake Luja Makingo, ambapo hakumkuta na kuamua kufungua nyumba yake kisha kuingia ndani na watoto na kuanza kufanya  mauaji hayo.

Amesema kuwa miili ya marehemu hao ilikutwa yote ndani ya chumba kimoja nyumbani kwa Luja Makigo, huku kisu kinachosadikika kutumika katika kutekeleza tukio hilo kikiwa kimebaki shingoni kwenye mwili wa mama huyo.

Ameeleza kuwa Makingo baada ya kurejea nyumbani kwake akitokea hospitali alipokwenda kwa ajili ya matibabu, ndipo alipobaini tukio hilo na kutoa taarifa kwa vongozi.

“Chanzo cha tukio ni ugonjwa wa akili, kwani ndugu huyo wa marehemu ameeleza kuwa dada yake amekuwa akisumbuliwa na tatizo hilo la ugonjwa wa akili kwa muda mrefu na alishawahi kufanya jaribio la kujiua kwa kujichana shingoni kwa kutumia kiwembe miaka kadhaa iliyopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles