24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Asasi za kiraia kufanya utafiti

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

WAKATI wiki ya Azaki ikitarajiwa kuanza  kesho jijini Dodoma ,Mkurugenzi  Mkazi wa Shirika la  Christian Blind Mission (CBM),Nesia Mahenge amesema asasi za kiraia zipo katika mchakato wa kufanya  utafiti  wa kujua ni mchango gani   wameutoa katika shughuli mbalimbali.

Amesema utafiti huo utasaidia  kutoa picha kamili kuweza  kuonesha mchango ambao asasi za kiraia wanautoa kwa nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 22,2021,mkurugenzi huyo amesema kuna mambo mengi ambayo asasi za kiraia zimefanya kuanzia ngazi ya Taifa hadi kijijini ikiwa ni pamoja na kusomesha wataalamu na kutoa huduma mbalimbali.

Amesema wamekuwa wakifanya shughuli za  kuleta maendeleo  kwa kushirkiana na Serikali  na wamepewa   miongozo katika kuingia  ubia wa  kuleta maendeleo.

Amesema wanafanya shughuli katika sekta za  elimu,kilimo,afya na masuala ya ajira, kuwajengea uwezo na maeneo mengine.

“Na kuna tafiti  tunataka kuufanya na  tumeishaanza mchakato kuweza kuangalia kwa takwimu maalum ni michango ya kiasi gani kama ni rasilimali fedha,watu,vifaa mbalimbali ambavyo vinatolewa  na huduma ambazo zinatolewa  kuweza kujua tumefanya kwa kiasi gani.

“Nadhani huo utafiti utasaidia sana kutoa picha kamili kuweza  kuonesha mchango ambao tunatoa Tanzania,”amesema

Katika hatua nyingine,Mkurugenzi huyo amesema Spika  wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kesho anatarajia kufungua wiki ya Asasi za Kiraia(AZAKI) Mkoani Dodoma ambapo jumla ya Asasi zaidi ya 150 zitashiriki katika maonyesho  lengo likiwa ni kuonyesha mchango wake katika maendeleo ya Taifa. 

Amesema,pamoja na mambo mengine wiki hiyo inawaleta wadau mbalimbali wa Maendeleo nchini ikiwemo wananchi,Serikali,AZAKI na sekta binafsi  ambao wote kwa pamoja watajadili na kusherehekea mchango wa AZAKI katika kuleta maendeleo nchini.

“Tunawaita wadau mbalimbali wa maendeleo kujumuika nasi kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo   ushauri wa kisheria,kufahamu kazi tunazofanya na kusherehekea kwa pamoja ,”amesema.

Amesema  uzinduzi huo wa wiki ya AZAKI utahudhiriwa na wahisani wa maendeleo wakiwemo ubalozi wa Denmark Utakaowakilishwa na Sascha Mulla na Ubalozi wa Canada útawakikishwa na Ms.Helen Fytche.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa United Nations Association (UNA) Reynald Maeda amewataja viongozi na wageni kutoka Serikalini watakaoshiriki katika uzinduzi huo ni pmaoja na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri,Meya wa Jiji la Dodoma Prof.Davis Mwamfupe na mwakili kutoka Wizara ya Afya Vickness Mayao.

“Katika kusherehekea mafanikio  ya sekta ya AZAKI na ubia Wetu baina ya wananchi maonyesho yatakayofanyika tarehe 23 hadi 24 Oktoba katika ukumbi wa Jakaya Kikwete na kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali kama Profesa Jay,Sheta,Barnabas,Gnako,na wasanii wa Dodoma,”amesema.

Amesema  kuwa wiki ya AZAKI hukutanisha wadau wa maendeleo kujadili masuala ya masingi kuhusu ustawi wa sekta pamoja na maendeleo ya Taifa Kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles