24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kirikuuu za NMB Bonge la Mpango zatua Mbalizi, Mpanda

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

AWAMU ya Pili ya Kampeni ya Weka Akiba na Ushinde inayoendeshwa na Benki ya NMB ‘NMB Bonge la Mpango – 2merudi Tena,’ imezidi kushika kasi, baada ya droo ya pili kufanyika, ambako Melkiadi Kepa wa Usongwe, Mbeya na Anthony Meshack wa Mpanda mkoani Rukwa, wametangazwa washindi wa pikipiki za miguu mitatu aina ya Sky Mark.

NMB Bonge la Mpango ni kampeni itakayoendeshwa kwa kipindi cha wiki 12, ikilenga kuhamasisha utamaduni chanya wa kujiwekea akiba, ambako washindi 50 watajinyakulia pikipiki za mizigo 50 zenye thamani ya Sh milioni 225, huku washindi 120 wakitarajia kujishindia fedha taslimu kiasi cha Sh milioni 12.

Afisa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Neema Kazoviyo (wa pili kushoto), akizungumza na mmoja wa washindi wa  droo ya Pili ya Kampeni ya Weka Akiba na Ushinde ‘NMB Bonge la Mpango – 2merudi Tena’ iliyofanyika katika tawi la NMB Magomeni jijini Dar es Salaam jana. Kulia anayeshuhudia ni Afisa Mwandamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Pendo Mfuru na wa pili kulia ni Meneja wa NMB tawi la Magomeni, Mary Marungi. (Na Mpiga Picha Wetu).

Droo hiyo ya NMB Bonge la Mpango (Awamu ya Pili), imefanyika Ofisi za NMB Tawi la Magomeni jijini Dar es Salaam, ambako Melkiadi wa NMB Tawi la Mbalizi Road na Anthony wa Tawi la Mpanda, ni kati ya washindi 12, ambako 10 miongoni mwao walishinda pesa taslimu Sh 100,000 kila mmoja, Pikipiki mbili za Sky Mark ina thamani ya Sh milioni 4.5.

Akizungumza kabla ya kuchezeshwa kwa droo hiyo, Meneja wa NMB, Tawi la Magomeni, Mary Marungi, alisema NMB Bonge la Mpango ni kampeni ya kimkakati, inayolenga kuhamasisha utamaduni chanya wa kutumia huduma za kibenki kwa kuweka ili kuwezesha utimilifu wa malengo ya mtu mmoja mmoja, kikundi ama taasisi.

“Kampeni hii imezinduliwa Oktoba hii mwanzoni na itadumu Hadi Desemba, ambako kila wiki tutakuwa tukiwazawadia washindi 12, kati yao 10 watashinda pesa taslimu na wawili wanajinyakulia pikipiki za miguu mitatu aina ya Sky Mark zenye thamani ya Sh milioni 4.5 kila moja.

“Ili kushindania zawadi hizo, mteja mwenye akaunti anapaswa kuweka akiba isiyopungua Sh 100,000 na yule ambaye hana akaunti, anatakiwa kufungua na kuweka akiba isiyokuwa chini ya kiasi hicho na moja kwa moja ataingia katika drop zetu hizi za kila wiki.

“Wito wetu kwao ni kuwataka waendelee kuweka akiba, ambapo licha ya kuwa njia ya kuwawezesha kufanikisha malengo yao, pia itawapa nafasi ya kujishindia zawadi hizi muhimu, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho we mwaka na mwanzo wa mwaka ujao, ambako kunakuwa na sikukuu na pia malipo mbalimbali ya ada za watoto mashuleni,” alisema Marungi.

Aidha, Marungi aliongeza kuwa, kila mtu anapaswa kuishi kwa malengo na kuwa kujiwekea akiba ni kati ya siri ya mafanikio ya walio wengi, hivyo njia sahihi ya kufanikiwa ni kuitumia kampeni ya NMB Bonge la Mpango kujiwekea akiba na kufanikisha malengo ya muda mrefu na muda mfupi.

Droo hiyo ilichezeshwa mbele ya Pendo Albert Mfuru, ambaye ni Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), aliyesema jukumu lake katika tukio hilo ni kuhakikisha vigezo na masharti yanayosimamia michezo hiyo vinafuatwa, huku akiwahakikishia wateja wa NMB kuwa bahati nasibu hiyo inaendeshwa kihalali na washindi wake wanapatikana bila upendeleo wowote.

Washindi 10 walioibuka na zawadi ya pesa taslimu katika droo hiyo ni pamoja na Keneth Mkumbo, Hadija Abbi, Rose Nungu, Nesha Mlaki, Selina Mwalugaja, Mwanahamisi Mwingira, Ado Mbunda, Dismas Simsonga, Emmanuel Kirenga na Shabani Kalinga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles