27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Malikia, shetani wa ujangili mbaroni

MAGHEMBEENa Ramadhan Libenanga, Morogoro

SERIKALI imesema imekamata vinara sita wa ujangili wakiwamo wawili wanaojulikana kwa majina ya ‘shetani na ‘malikia’ ambao walikuwa wakisakwa kwa  muda mrefu.

Mbali ya vinara hao ambao majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za  usalama, pia msako mkali unaendelea dhidi ya majangili nane.

Akizungumza wakati wa kufungua wa mkutano wa mwaka wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na wahariri  na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari mjini Morogoro jana, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe  alisema kukamatwa kwa majangili kunatokana na mkakati wa wizara kuhusu  vita  dhidi ya ujangili.

“Tumefanikiwa kukamata shetani na malkia wa ujangili ambao kwa kweli wamekuwa vinara wa ujangili…wapo wenzao wanane ambao wanaendelea kutafutwa, naamini tutawakamata tu,”alisema Waziri Maghembe.

Alisema vita dhidi ya ujangili hivi sasa inapiganwa kwa ushirikiano mkubwa wa nchi za Jumuiya za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), kwa vile tatizo hilo limekuwa mtambuka.

Baada ya kuona tatizo hilo linashamiri, Serikali imeamua kupeleka taarifa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN)  isaidie kuzibana baadhi ya nchi ambazo zimekuwa vinara wa kununua pembe za ndovu, ikiwamo   China.

“Baada ya kuona vita hii ni kubwa tumelazimika kupeleka kilio chetu pale UN watusaidie kuwabana wanunuzi wakubwa ambao wamekuwa wakitoa fedha nyingi kwa ya biashara hii.

“Pamoja hawa wakubwa wana nafasi kubwa na mchango mkubwa wa kusaidia tatizo hili, maana fedha zinatokea kwao,”alisema Waziri Maghembe.

Alisema pamoja na hatua hizo, bado tatizo la mauaji ya wanyama  kama tembo, faru na simba bado ni kubwa.

Kuhusu changamoto katika hifadhi za taifa, Waziri Maghembe alisema limekuwapo  wimbi kubwa la uingizaji wa mifugo ambayo inahatarisha uhai wa wanyamapori.

“Hivi sasa tuna sheria ya kuzuia mifugo kuingia ndani ya hifadhi,” alisema.

Akizungumzia idadi ya watalii waliongia nchini kuanzia Januari hadi Desemba 2015, alisema waliingia milioni 1.1, huku wizara ikipata Dola za Marekani  bilioni 2.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi alisema vyombo vya habari vina jukumu la  kufichua mitandao ya ujangili, uharibifu wa misitu   na vitendo visivyokubalika katika hifadhi za taifa.

Alisema kuna kila sababu Watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vilivyopo ili kujenga utalii wa ndani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles