24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani kuipa Tanzania Dola milioni 800

Pg 2Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

SERIKALI ya Marekani imesema itatoa dola milioni 800 kwa Tanzania kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa ilieleza kuwa Balozi wa Marekani nchini Tanzania,  Mark Childress alikuwa na mazungumzo na Rais Dk. John Magufuli   Dar es Salaam jana.

Childress alisema kutolewa kwa fedha hizo ni uthibitisho kuwa kutotolewa kwa fedha za awamu ya pili ya mradi wa changamoto za milenia (MCC-2) hakujaondoa uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na Marekani ikiwamo utoaji wa misaada ya maendeleo.

“Tumezungumza mambo kadhaa na wiki hii Tanzania na Marekani kupitia shirika letu la misaada la USAID.

“Tunatarajia kutiliana saini mkataba wa zaidi ya dola milioni 400 kwa ajili ya mwaka ujao, pia tumezungumza kuwa kutakuwa na dola milioni 800 zitakazotolewa na Marekani kwa ajili ya miradi mbalimbali na hii haihusiani na MCC.

“Ukweli ni kwamba tunayo mengi ya kufanya pamoja katika sekta mbalimbali ikiwamo afya, elimu na kilimo na tutafanya kila juhudi kuhakikisha haya yanafanikiwa,”alisema Balozi Childress muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo na Rais Magufuli.

Naye Rais Dk. Magufuli alisema Serikali ya awamu ya tano itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano na Marekani na   fedha za msaada  Marekani ni muhimu kwa maendeleo ya Tanzania.

“Amekuja kutuhakikishia kwamba watatoa fedha kwa ajili ya Tanzania na anasema sasa hivi watatoa zaidi ya dola milioni 800, na mkataba mwingine tunaweza tukasaini hata kesho wa dola milioni 410.

“Pia ametuhakikishia kwamba kutotoa fedha za MCC hakuna maana ya kupotea kwa urafiki kati ya Tanzania na Marekani. Urafiki wa Tanzania na marekani upo pale pale na sasa wanaongeza fedha  nyingi zaidi katika kuonyesha kwamba juhudi za ‘hapa kazi tu’ zinaendelea,” alisema Rais Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles