24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Makonda awavaa watumishi wa umma

paul-makondaNa MWANDISHI WETU – Dar es Salaam

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema watumishi wa umma wanapiga majungu na hawafanyi kazi.

Kauli hiyo aliitoa jana alipoanza ziara yake ya siku 10 mkoani hapa kwa kutembelea Wilaya ya Kigamboni.

Alisema nia ya ziara hiyo ni kugundua kero za wananchi pamoja kuwahamasisha wafanyakazi wa Serikali kuwajibika.

“Nataka wafanyakazi wafanye kazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya rais wetu, nimegundua asilimia 80 ya wafanyakazi wa Serikali hawafanyi kazi, asilimia 80 ya watumishi wa umma hawafanyi kazi, wanapiga majungu, wanasoma magazeti, ni wambea. Kilichobaki ni kusubiri mwisho wa mwezi kwa ajili ya mshahara,” alisema Makonda.

Alisema hataki kuona wananchi wakikimbilia kwake kuomba msaada wa utatuzi wa changamoto zao wakati Serikali ina wafanyakazi kuanzia ngazi ya vitongoji.

Pia alipiga marufuku shughuli za uchimbaji wa mchanga katika makazi ya watu.

Akizungumza wilayani hapa baada ya kutembelea mitaa ya Maweni na Mjimwema ambako alijionea uharibifu uliotokana na uchimbaji huo, pia alisema kila baada ya miezi mitatu kutakuwa na mkutano wa ma-DC watakaoulizwa maswali na wananchi kuhusu walichokifanya.

“Wapo watu wengine wanajenga barabara, wanatumia haya machimbo kujenga barabara, si vyema kukamilisha barabara ya lami halafu mkatuachia mahandaki kama haya, nayo ni marufuku, watafute sehemu nyingine,” alisema Makonda.

Katika hatua nyingine, alisema tayari wamepatikana wadau watakaoanza kujenga vituo 10 vya polisi kuanzia mwezi ujao.

Awali, Makonda alizungumza na viongozi wa wilaya hiyo pamoja na kuzindua mpango mkakati wa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles