PYONGYANG, Korea Kusini
KITENDO cha Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence kuifananisha Korea Kaskazini na Libya kimezidi kuchafua uwezekano wa Rais wake na Doland Trump na mwenzake,Kim Jong-un ambao walitarajiwa kukutana Juni 16 mwaka huu.
Kauli hiyo imeonekana kuwa ni dharau kwao na kumfanya Ofisa wa cheo cha juu  katika Serikali ya  Korea Kaskazini amemjia juu  Pence na kumuita  “mjinga”  na huku ikimuonya kuwa yanaweza kuibuka  maonyeshano ya ubabe wa nyuklia ikiwa mazungumzo yatashindwa kufanyika kutokana na kauli zake za dharau.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Â Son-hui alisema, Pyongyang haitaweza kuibembeleza Marekani kwa ajili ya mazungumzo hayo.
“Kama mtu ambaye nimehusika kwenye masuala ya Marekani, siwezi kuficha mshangao wangu kufuatia matamshi kama hayo ya ‘kijinga’ yanayotoka kinywani mwa Makamu wa Rais wa Marekani,” alisema, Son-hui
“Ikiwa Marekani itakutana nasi au kutukabili kinyuklia inafuatia na uamuzi na tabia za Marekani.”
Choe alisema tangu mwanzo, Pyongyang haikuwa inabembeleza kufanyika mazungumzo na akasema kuwa hawatakubali kuona wanadhalilishwa kwa kiasi hicho.
Kauli hiyo ya Makamu huyo wa Trump, imekuja pia wakati  Mshauri wa Masuala ya Ulinzi wa Marekan,i John Bolton naye wiki iliyopita kuikasirisha Korea Kaskazini  kwa kusema kuwa utatumiwa mfumo wa Libya katika kuondoa zana za nyuklia.
Siku za hivi karibuni pande hizo mbili zimeonya kuwa mkutano wa Juni 12 mwaka huu  unaweza kuharishwa au kufutwa kabisa.
Rais wa Marekani Donald Trump mapema wiki hii  pia alisema Korea Kaskazini ndiyo ingetimiza masharti ya kufanyika kwa mazungumzo hayo.