31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

ALIYETAKA KUMPINDUA CASTRO AFARIKI

FLORIDA, Marekani


KACHERO wa zamani wa kundi la kijasusi la Marekani CIA ambaye kwa miaka mingi alikuwa akijari kuipindua Serikaliya Cuba,  Luis Posada Carriles,  amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC, kachero huyo alifariki usiku wa kuamkia jana  mjini Florida  na kwa mujibu wa wakili wake alikuwa akiugua  saratani ya koo..

Carriles alikuwa mmoja wa maadui wakubwa wa rais wa zamani wa Cuba Fidel Casto na aliwahi kushiriki  katika uvamizi ulioungwa mkono na Marekani mwaka 1961 na analaumiwa kwa kuiangusha ndege ya abiria.

Hata hivyo licha ya kutajwa  kuwa gaidi nchini Cuba, lakini  alionekana kama shujaa miongoni mwa raia wengi wa nchi hiyo  waliokuwa uhamishoni.

Mwandishi wa BBC nchini Cuba anasema, Carriles alikuwa mtu aliyechukiwa sana nchini  humo kwa kuhusika katika kuilipua ndege ya abiria  mwaka 1976 na kusababisha vifo vya watu wote 73 waliokuwamo.

Wakati wa kuangunshwa ndege hiyo, Carriles alikuwa akiishi nchini Venezuela ambapo alikuwa akifanya kazi kama jasusi katika idara ya ujasusi nchini humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles