24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Makala| TaCRI yawajengea uwezo wakulima wa kahawa 377,496

Safina Sarwatt, Arusha

Taasisi ya Utafiti wa Kahawa nchini (TaCRI) imetoa mafunzo ya kanuni bora za kilimo cha kahawa na uzalishaji miche kwa wakulima 377,496 kwa lengo kuongeza uzalishaji wa kahawa inayokubalika katika soko la dunia.

Wanahabari wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa COSTECH wakati wa warsha hiyo.

Sambamba na mafunzo pia wamepanua mashamba ya mbengu ili kugawa kwa vikundi vya wakulima mbegu bora zinazokinzana na magonjwa ya kutu ya majani.

Leonard Kiwelu ni Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kahawa nchini (TaCRI) anabainisha hayo katika warsha ya kuwajengea uwezo Wandishi wa Habari wa Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika jijini Arusha yakiratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifuni (COSTECH).

“Katika kukabiliana na changamoto hii, tumepanua mashamba yetu ya mbegu ili vikundi vya wakulima vipelekewe mbegu (na utaalam wa kuzi Mafunzo ya kanuni bora za kilimo cha kahawa na uzalishaji miche yametolewa kwa wakulima wa kahawa 377,496,” anasema Kiwelu.

Anabainisha kuwa tayari Maafisa Ugani 10,865 wamepata mafunzo juu ya kanuni bora za kahawa, ambapo zaidi wakulima wahamasishaji 3,849 wamepata mafunzo nchi nzima.

Anaongeza kuwa taasisi hiyo imefakiwa kuanzisha bustani 400 za kuzalisha miche bora chotara ya kahawa, Robusta na Arabika ambazo zimeanzishwa nchi nzima .

“Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali jumla ya miche 51,323,308 ya aina bora chotara ya kahawa imezalishwa (inayotosheleza Hekta 38,560) na kusambazwa kwa wakulima kwa ajili ya kuotesha mashambani, pia kuanzisha bustani mama,” anasema Kiwelu.

Kwa mujibu wa utafiti wa taasisi hiyo tayari maeneo ya upanuzi wa kilimo cha kahawa na kutambua rutuba ya udongo imekamilika katika mikoa 17 nchini nakwamba eneo hili linahusu rutuba ya udongo na lishe ya mimea, udhibiti wa visumbufu na makuzi ya mimea. 

Anaitaja mikoa hiyo kuwa ni Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya na Songwe, (ambapo walishirikishwa katika mradi wa Bodi ya Kahawa) na Mikoa ya Rukwa, Katavi, Kigoma, Kagera, Mara, Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Geita, Mwanza na Morogoro imeweza kunufaika na mradi huo.

 Amesema taarifa za msingi za rutuba ya udongo katika mikoa hizo zimewasilishwa kwenye halmashauri husika kwa matumizi ya maafisa ugani, pamoja na mapendekezo ya namna bora ya kutunza rutuba mashambani. 

“TaCRI imefanya upanuzi wa eneo jipya lenye  zaidi ya hekta 15,000. Inawahamasisha wakulima kupima udongo wa mashamba yao ili kufahamu tabia zake na inayo maabara ya kisasa kwa ajili hiyo.

“Tulianzisha bustani ya viuatilifu asilia mwaka 2003 ikiwa na Utupa (Tephrosia vogelii) na Mwarobaini (Azadirachta indica). Kufikia 2007, bustani ilishapanuka kufikia hekta moja, ikiwa na aina 8 za mimea,”amesema Kiwelu.

Amesema katika majaribio matatu ya kimaabara yalifanyika dhidi ya kimatira mwaka 2010 na ikaonekana kwamba kipimo cha chini cha gramu 1,200 kwa lita kilikaribiana na rejea (Selecron). 

“Tafiti za mitego ya ruhuka (CBB) zimeonyesha kuwa mchanganyiko wa 1:1 wa spiriti na maji, pamoja na vileo vya kienyeji kama mbege, dengelua, ulanzi na rubisi, vina uwezo mkubwa kama chambo cha kuwatega ruhuka,”amesema Kiwelu.

Ameongeza kuwa teknolojia hiyo imeshaanza kuzoeleka miongoni mwa wakulima wadogo na wakubwa. 

“Pia kiuatilifu cha Fipronil kilitafitiwa na kupendekezwa katika kudhibiti bungua weupe wa kahawa (WCSB) ambao wamekuwa ni tishio kwa tasnia ya kahawa katika maeneo mengi nchini,”amesema.

Kwa upande wa makuzi ya kahawa, tuliweza kubuni mtindo wa 3:1 wa kilimo-mseto cha kahawa na migomba kwa aina ndefu (mistari 3 ya kahawa ndani ya mistari 2 ya migomba) mwaka 2004; na 4:1 kwa aina fupi (mistari 4 ya kahawa ndani ya mistari 2 ya migomba) mwaka 2021.

Nao baadhi ya wakulima wa kahawa kutoka kata ya Kilomeni Mwanga mkoani Kilimanjaro wamesema tayari wamepatiwa mafunzo pamoja na miche bora chotara ambayo zinakinzana na magonjwa ya kutu ya majani.

Makamu mwenyekiti halmashauri ya wilaya ya Mwanga na diwani wa kata ya Kilome mwalimu Abdallah Mgala amesema tayari wamepatiwa miche 6000 na taasisi ya utafiti wa kahawa nchini (TaCRI) na kwamba wanatarajia kuvuna kahawa bora ambayo inakubalika katika soko la ndani na nje.

Amesema mikakati yao nikuwatumia watafiti wa kilimo kuanzisha mashamba darasa na bustani za kuzalisha miche ili waweze kusambaza kwa wakulima wa kahawa.

Amesema pia wanakusudia kuanzisha chama cha msingi cha ushirika katika kata hiyo ili wakulima watakaopzalisha kahawa zao waweze kupata soko la uhakika na bei nzuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles