23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati ya bunge ya Ardhi yaridhishwa na utekelezaji wa mradi wa upimaji viwanja Nyafula

*Ni jimbo la Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Dk. Angeline Mabula

Na Clara Matimo, Mwanza

Kamati ya Kuduma ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Machi 16, imefanya ziara  katika eneo la nyafula  kata ya Sangabuye ambako mradi wa upimaji viwanja 1,726 kwa gharama ya Sh milioni 48.7 unatakalezwa na Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza na kuridhishwa na utelelezaji wake.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo wakiangalia utekelezaji wa zoezi hilo,

Waziri wa Wizara ya  Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula, amesema, lengo la mradi huo wa kupanga, kupima na kumilikisha ardhi ni kufanikisha utekelezaji wa mpango kabambe wa jiji la Mwanza wa  mwaka 2015/2035 kwa kulipanga jiji lote.

Dk. Mabula ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemema mkaoni Mwanza(CCM) amewaambia wajumbe wa kamati hiyo kwamba mradi huo ukikamilika utafanya eneo lililopangwa na kupimwa kwa manispaa hiyo kufikia asilimia 86.

“Waheshimiwa wajumbe wa kamati hii ukiondoa  visiwa eneo lililopangwa na kupimwa ni asilimia 90 ya ardhi yote katika Manispaa ya  Ilemela lengo letu ni kupima na kumilikisha ardhi wananchi kwa asilimia 100 ifikapo 2025, eneo kubwa limepangwa kupitia miradi ya serikali, upimaji binafsi pamoja na urasimishaji ardhi.

“Mradi wa kupanga, kupima na kumilikisha viwanja unatekelezwa katika Kata za Sangabuye, Bugogwa na Shibula,  ukikamilika utafanikisha mambo mbalimbali ikiwemo kutanua wigo wa mapato ya serikali kuu yatokanayo na kodi ya ardhi,  kupanua mji na kuhakikisha maeneo yanayopangwa na kumilikishwa yanafikika kwa miundombinu ya barabara, umeme na maji,“ amesema Dk. Mabula.

Baada ya kukagua mradi huo wajumbe wa kamati hiyo akiwemo Hawa Mwaifunga (Chadema), walisema wameridhishwa na utekelezaji wa mradi na kushauri  halmashauri zingine zifike katika manispaa hiyo ili zijifunze namna bora ya kutekeleza miradi hiyo.  

“Manispaa ya Ilemela ni mfano mzuri sana, mheshimiwa waziri wa wizara ya ardhi naomba nikupongeze sana kutoka moyoni,  mimi  ni mbunge wa upinzani huwa sina kawaida ya kupongeza pongeza lakini kutokana na kazi kubwa na nzuri unayoifanya naomba nikupongeza kutoka moyoni wewe na watendaji wote wa wizara yako  kwa kufanya kazi  nzuri sana.

 “Commitment uliyonayo wewe  waziri kwa kamati yako,  mmekuwa mkisikiliza na kufuata ushauri ambao tunawashauri  ndiyo maana mmekuwa mkifanya kazi nzuri sana, kwa kweli tunakosa hata maswali ya kuwauliza, hongereni sana,”mesema Mwaifunga.

Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Ally Makoa, alisema katika halmashauri na manispaa zote ambazo wamepita kukagua miradi ya ardhi  Ilemela imeongoza kiutendaji huku akimpongeza Mkuu wa Idara ya Mipango Miji na Ardhi wa manispaa hiyo, Shukrani Kyando, pamoja na viongozi wengine wa mkoa na wilaya hiyo kwa kufanya kazi kwa ushirikiano ambapo alibainisha  kwamba umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles