28.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Makala: ‘MICROBIOLOJIA’ uoteshaji vimelea vya magonjwa unavyofanikisha uchunguzi wa dawa na vipukusi-2

Na Aveline Kitomary

‘Microbilojia’ hii ni Sayansi ya utafiti wa viumbe vidogo kama vile bakteria visivyooneka kwa macho ya kawaida ila kwa kutumia microscope, viumbe hivi vidogo (micro-organism) vinaweza kuishi sehemu yoyote Ulimwenguni, licha ya kuwa na madhara wakati mwingine lakini pia huwa uwepo wake ni muhimu kulingana na mazingira husika.

Katika maabara mbalimbali hufanyika ‘Micro bio challenge test’ hii humaanisha uwezo wa sampuli kuua vimelea au wadudu waliokusudiwa.

Mchunguzi wa Microbiolojia kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa, Waridi Msumari, anasema kwa kutumia maabara ya microbilojia wanaangalia uchafuzi wa vimelea unaoweza kutokea katika bidhaa zote zinavyodhibitiwa na Mamlaka kama dawa, vifaa tiba, vitendanishi na vipukusi.

Mchunguzi wa Maabara, Msumari Waridi awaonesha waandishi wa habari jinsi ya kuhesabu vimelea vilivyoota.

MICROBIOLOJIA YA DAWA

Waridi anasema kwa upande wa dawa kuna aina tofauti tofauti za chunguzi zinazoweza kufanyika kulingana na aina ya dawa.

“Mfano  dawa ambazo hazipaswi kabisa kuwa na  vimelea vya wadudu (Sterile Products) ni kama vile dawa za sindano (injection) hizi hufanyiwa test inayoitwa ‘sterility test’ pamoja na ‘bacterial endotoxin test’ ili kuangalia kama kuna uchafuzi wowote uliotokea wakati wa utayarishaji wa dawa hizo.

“Vilevile tunafanya uchunguzi   wa  ‘non sterile products’ mfano dawa za vidonge kuangalia kiwango cha wadudu waliopo kwa kufanya ‘Microbial limit test’ pia tunaangalia ni aina gani vimelea waliopo (Specific tes).

 “Hata kwenye midomo yetu, tumbo, koo kuna wadudu/ vimelea ambao hawana madhara (non pathogenic) katika kiasi ambacho wadudu hao hawawezi kusababisha madhara mwilini lakini pia kuna aina ya vimelea vinavyosababisha magonjwa (pathogenic) hawapaswi kabisa kuwepo mwilini,” anasema Waridi.

Anabainisha kuwa endapo dawa (non sterile products) itakuwa na wadudu iwe kwa kiwango ambacho kimeruhusiwa hivyo mtumiaji hawezi kupata madhara.

“Tukishagundua dawa hiyo inakiasi gani cha wadudu tunaenda kufanya ulinganishaji na mwongozo uliowekwa kimataifa (pharmacopoeia) ili kujua dawa hiyo kama inafaa kwa matumizi au haifai.

“Mfano sisi tunaweza kukuta wadudu 200 na kwenye mwongozo wanasema wadudu hawapaswi kuzidi 100, hapa tunasema dawa imefeli   lakini kama utakuta mwongozo unasema ni wadudu wasizidi 100 halafu  tukakuta kwenye dawa kuna wadudu 80 tunasema sampuli imefaulu kigezo hicho.

“Lakini hapo hapo unaweza kuchunguza uwepo wa wadudu ambao hawatakiwi kuwepo kabisa (specific pathogen) japo kuwa inawezekana dawa ni kati ya zile ‘non sterile products’ lakini wadudu ambao husababisha magonjwa (pathogenic) hawatakiwi kuwepo unaangali kama wapo au hawapo.

Microbioloji kwenye dawa pia inaangalia uwezo wa dawa kuua  vimelea vinavyolengwa.

Mchunguzi wa Maabara, Msumari Waridi akionesha kemikali ya kupima sampuli (culture media)

Waridi anasema zipo hatua ambazo zinatakiwa kufuatwa ili kuweza kujua uwezo wa dawa kuua wadudu.

“Hii tunaiita (bioassay) unaangalia uwezo wa dawa kuua wale wadudu  mfano antibiotic unaweza kuchukua dawa ukaiandaa kwa jinsi muongozo wa uchunguzi unavyosema kishaunaweka  mdudu kwenye dawa hiyo  katika mfumo maalum kama inavyoelekezwa kwenye miongozo ya uchunguzi ili kujua kama dawa hiyo inafanya kazi iliyotarajiwa kwa kiwango gani,” anasema Waridi.

MANUFAA YA UCHUNGUZI

Waridi anasema manufaa ya uchunguzi wa microbiolojia ni kuhakikisha kuwa jamii inakuwa salama  kwa kutumia bidhaa ambazo zinaubora,usalama na ufanisi unaotakiwa.

 “Bidhaa zote  zinazothibitiwa na Mamlaka tunauhakika kuwa ni salama kwasababu zinapitia mchakato wa usajili na ili usajili ufanyike lazima ulete sampuli ambazo sisi tutazichunguza na kuhakikisha ubora na usalama wake.

“Hivyo jamii itakuwa salama kwasababu ya umahiri wetu katika kuchunguza bidhaa zote zinazo dhibitiwa na Mamlaka,”anafafanua Waridi.

TUNAPIMWA UMAHIRI

Waridi anasema kuwa kuna utaratibu wa kupima umahiri wa maabara umekuwa na nafasi kubwa ya kujiamini katika upimaji wa sampuli.

“Umahiri wa wachunguzi wa maabara unapimwa kwa kushiriki proficiency testing (PT) kutoka kwa waandaaji tofauti tofauti ulimwenguni.

“Kinachofanyika ni kwamba PT  provider anatoa sampuli ambayo yeye anajua majibu yake, lakini sisi washiriki hatujui majibu ya hiyo sampuli, anazigawa kwa washiriki walioomba kujipima umahiri ili waweze kufanya uchunguzi kulingana na utaratibu wa maaabara yao.

“Wakishamaliza kufanya uchunguzi, majibu ya sampuli hiyo ya PT  yanapelekwa kwa PT provider na baada ya kukusanya majibu yote ya washiriki PT provider anajumuisha majibu hayo na kuyatoa majibu sahihi na hivyo kila mshiriki anaweza kujua kama amefaulu ama amefeli kwa kulinganisha majibu yake na majibu sahihi yanayotolewa na PT provder,” anasema Waridi.

Anasema majibu hayo yanaweza kumjenga mchunguzi kwa kuweza kugundua mapungufu yaliopo na kuweza kuyafanyia marekebisho ili kuwa na ujuzi zaidi.

“Anaweza, utaratibu wetu ni kwamba kila mchunguzi ni  lazima afanye PT angalau moja kwa mwaka na kama majibu yakija amefeli ni lazima ujiulize kwa nini amefeli kama maabara pia inafatiali kwanini huyu amefeli ili aweze kujengewa uwezo katika eneo hilo.

“Hizo PT zinatusaidia kuimarisha umahiri wa wachunguzi ,inajenga kujiamini kwamba majibu yanayotoka katika maabara yetu ni sahihi  kwasababu kama PT imetoka huko Duniani tukafanya katika mazingira yetu na tukafaulu inamaana tutakuwa na uhakika zaidi na maabara yetu,”anahitimisha Waridi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles