28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

MAJAMBAZI WANNE WAUAWA DAR

MARGRETH MWANGAMBAKU (TUDARCO) Na LEONARD MANG’OHA

-DAR ES SALAAM

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limewaua majambazi wanne ambao walikuwa kwenye tukio la uvamizi eneo la Kigogo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 2 usiku.

Alisema kuwa walifanikiwa kuzima uhalifu wa majambazi hao baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.

“Majambazi hao walikuwa sita na bunduki mbili aina ya SMG na bastola. Mara baada ya kufika, askari walitoa amri ya kujisalimisha na majambazi hao walikaidi na kuanza kurusha risasi ovyo.

“Askari baada ya kuona hivyo walijibu mashambulizi na kufanikiwa kuwajeruhi majambazi wanne kwa risasi na majambazi wawili walifanikiwa kukimbia,” alisema Mambosasa.

Alisema katika mapambano hayo, majambazi waliojeruhiwa walikamatwa wakiwa na bastola aina ya Chinese yenye namba 16014877 ikiwa na risasi saba.

Kamanda Mambosasa alisema majambazi hao waliojeruhiwa walipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na wote wanne walifariki dunia wakiendelea kupata matibabu.

Hata hivyo, Kamanda Mambosasa hakuwataja majina waliofariki dunia wala pikipiki zilizokamatwa kwa kile alichoeleza kuwa ni sababu za kiuchunguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles