29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

WAKIMBIZI 12,000 WAOMBA KUREJESHWA MAKWAO

Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM

WAKIMBIZI walioomba kurejeshwa makwao kwa hiyari wamefikia 12,000 na wanatarajia kuanza kurejeshwa wiki ijayo kuanzia Sept 7, mwaka huu.

Hadi sasa wakimbizi waliopo nchini ni 351,400 ambao wanatoka Burundi (277,535), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (73,000), Wabantu kutoka Somalia (150) na mataifa mengine 338.

Akizungumza jana wakati wa kikao cha pamoja baina ya serikali ya Tanzania, Burundi na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, alisema serikali haitatumia nguvu kuwarejesha wakimbizi hao.

“Tumetunza wakimbizi kuliko nchi yoyote ile hatuoni kwanini tutumie nguvu, tumeweka mkazo kama sheria inavyotaka kwamba mkimbizi anayetaka kurejea kwao kwa hiyari asaidiwe kurudi,” alisema Nchemba.

Alisema sheria za kimataifa zimeelekeza kama watu wanataka kurudi kwao kwa ridhaa yao ni jukumu la serikali katika nchi husika kuwasiliana na wadau wanaohusika na masuala ya wakimbizi kwa ajili ya kuwarejesha.

Kwa mujibu wa waziri huyo, wakimbizi waliopo nchini wanaishi katika kambi za Nyarugusu (142,172), Nduta (126,740), Mtendeli (50,063), Kigoma vijijini (23,047), makazi ya zamani (9,036), Lumasi (143) na Dar es Salaam (199).

Naye Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burundi, Pascal Barandagiye, alisema wamejiandaa kuwapokea wakimbizi wote watakaokuwa tayari kurejea kwani kwa sasa hali ya usalama nchini humo ni shwari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles