25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa aonya wamiliki, waendeshaji vituo yatima

Elizabeth Joachim, Dar es salaam

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amewataka wamiliki vituo vya kulelea watoto yatima kuacha kuwalea katika maadili yasiyofaa.
Kutokana na hali hiyo, amewataka maofisa ustawi wa jamii kuhusishwa katika usajili wa mtoto ili kuhakikisha watoto wanaostahili kuwekwa kwenye vituo hivyo wamesajiliwa.

Waziri Mkuu amesema hayo jana Jumapili Mei 26, Jijini Dar es Salaam, wakati wa futari ya pamoja na watoto yatima kutoka kwenye vituo sita vya kulea watoto yatima ikiwa ni pamoja na Ijango Zaida Orphanage Centre, Alzama Orphange Centre, Arusha Foundation, Madina Orphanage Centre Hiyari Orphanage Centre na Hisani Orphanage.

“Nitoe rai kwa mtu mmoja mmoja, watu, taasisi na makao wazingatie baadhi ya taratibu za msingi za uendeshaji wa makao kama vile mtoto kukuzwa katika mazingira ya familia, kuzingatia misingi ya kitaifa badala ya misingi ya tamaduni za kigeni.

“Mtoto kukuzwa kwa kuzingatia maslahi bora ya mtoto, kuzingatia umuhimu wa kuwa na mwendelezo katika dini ya mtoto na utamaduni wake, kutotenganisha watoto na ndugu na kuhakikisha watoto wote wanapata huduma stahiki, kulindwa dhidi ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji na kutunzwa na kuendelezwa hadi kufikia kimo cha utimilifu wao,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles