22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

P-Square kufikishana mahakamani

LAGOS, NIGERIA

NYOTA wa muziki nchini Nigeria, Peter Okoye, ameweka wazi kuwa anatarajia kwenda mahakamani kumshtaki ndugu yake, Paul Okoye, kwa kutumia picha zake kwa ajili ya kutangaza tamasha lake la muziki.

Inasemekana kuwa Paul na timu yake wanatarajia kufanya tamasha la muziki nchini Angola, hivyo amekuwa akitumia picha mbalimbali akiwa na ndugu yake huyo kwa ajili ya kutangaza tamasha hilo.

“Nashangaa kuona picha yangu wakiitumia kwa ajili ya kuuza kwenye tamasha lao huko nchini Angola bila ya ruhusa yangu, hivyo mwanasheria wangu atalifuatilia hilo mapema iwezekanavyo,” aliandika Peter.

Peter na Paul walikuwa wanaunda kundi la P-Square na kufanya vizuri duniani, lakini kundi hilo lilikuja kuvunjika kwa madai ya kutoheshimiana, lakini siku za hivi karibuni walidaiwa kumaliza tofauti zao, ila inaonekana kuwa mambo bado.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles