28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Airtel yatoa ufadhili kwa wanafunzi 130 wa VSOMO

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

KAMPUNI  ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia mradi wake wa kusaidia jamii, Airtel Tunakujali, imetoa ufadhali kwa wanafunzi 130 kuchukua masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kupitia applikesheni ya VSOMO.

Wanafunzi hao 130 wataweza kusoma moja ya kozi tano ambazo zinatolewa na VETA kulingana na changuo zao. Kozi hizo ni kozi za umeme, kozi za plumbing, kutengeneza keki, ufundi simu pamoja na kozi ya mapishi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza ufadhili huo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania, Beatrice Singano, alisema Kampuni ya Airtel imekuwa ikisaidia jamii kupitia mradi wa Airtel Tunakujali kwenye masuala ambayo yanagusa maisha yao ya kila siku.

Alisema Airtel Tunakujali ni mradi wa kusaidia jamii ambapo wanafanyakazi wa kampuni huchangia baadhi ya kipato chao na kuwekeza kwenye kusaidia jamii inayozunguka.

“Kwa maana hiyo, ufadhili ni kutokana na wafanyakazi wa Kitengo cha Masoko ambao waliandaa mbio fupi maarufu kama Fun run Januari mwaka huu. Lengo lilikuwa ni kufadhili wanafunzi 1,000 kwa mwaka mzima lakini kwa sasa tunaanza na hawa 130. Vijana hao watapa mafunzo ya ufundi stadi kwa nadharia kisha elimu ya vitendo kwa muda wa wiki moja kwenye Chuo cha VETA Kipawa au VETA Dodoma,” alisema Singano.

Singano alisema Airtel imeamua kuwafadhali vijana hao kupata elimu ya ufundi stadi, ikiwa ni moja ya njia ya kuwatengezea ajira.

“Nchi yetu kuna tatizo la ajira na hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa elimu ambayo inawafanya vijana kupata ajira. Kwa kuwafadhili vijana hawa ni kuwatengezea ajira lakini muhimu zaidi ni kuunga mkono kwenye uchumi wa viwanda,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa chuo cha VETA Kipawa, Sospeter Dickson, alitoa shukrani kwa Airtel kwa kufanikisha ufadhili huo wa vijana 130.

“Ni kweli kuna vijana wengi ambao wanapenda kujiunga na chuo chetu kupata elimu ya ufundi stadi lakini wanakosa karo. Hiki ambacho leo Airtel imekifanya ni cha kuungwa mkono lakini shukrani zaidi ziende kwa wafanyakazi ambao wamechangia fedha zao kufanikisha jambo hili. Sisi VETA tunaahidi kuendelea kutoa elimu bora ambayo itafanikisha vijana nchini kuweza kupata ajira,” alisema Dickson.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles