25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli asifu uimara wa JWTZ

1

Na JONAS MUSHU-PWANI

RAIS Dk. John Magufuli amesema hakuna anayeweza kuitisha Tanzania.

Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana baada ya kushuhudia maonyesho ya medani za kivita yaliyofanyika katika Kijiji cha Batini kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani na kuridhishwa na uimara wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) lililokuwa likisherehekea kilele cha miaka 52 ya kuanzishwa kwake.

“Kwa kile nilichokishuhudia Monduli, Arusha na nilichoshuhudia leo (jana) nimejiridhisha kabisa jeshi letu liko imara na hakuna mtu wa kutuchezea,” alisema Magufuli na kuongeza:

“Nchi yetu ina ukanda mrefu wa bahari zaidi ya kilomita 1,200 na nchi iliyozungukwa na nchi karibia tano lazima tuwe na jeshi imara na la mfano barani Afrika na hata duniani.”

Pia aliwapongeza marais waliopita kwa kuweka msingi mzuri wa uimara wa JWTZ huku akiahidi kuliboresha kwa kulifanya kuwa la kisasa na kuboresha maslahi ya wanajeshi.

Akizungumzia kuhusu kupenda kuteuwa wanajeshi katika nafasi mbalimbali serikalini, alisema anasukumwa na upendo wake kwa wanajeshi kutokana na sifa walizonazo za kuwa na maadili na kuchapa kazi.

“Watu wameanza kusema nataka kui-militarize Serikali lakini ukweli ni kwamba wanajeshi wana sifa nzuri ya maadili na uchapa kazi na hata wewe Mkuu wa Majeshi (Jenerali Davis Mwamunyange) ukistaafu nafasi zipo za kufanya kazi,” alisema Magufuli.

Katika hatua nyingine, aliwapa ajira vijana 70 kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Mgambo walioshiriki maonyesho ya medani hiyo.

“Nimeambiwa kuna vijana wa JKT 40 na mgambo 30 wameshiriki medani hii na kwa sababu mimi ni Amiri Jeshi Mkuu nimeona niwape ajira kuanzia leo (jana) wawe wanajeshi wa JWTZ,” alisema Magufuli.

Pia alivitaka vyombo vya ulinzi na JKT kujikita katika uzalishaji wa viwandani na ufanyaji wa biashara kwa maendeleo ya Taifa.

Kuhusu Gereza la Karagwe mkoani Kagera lililopata maafa kwa kubomoka baada ya kutokea tetemeko la ardhi hivi karibuni, alisema anasikitika kusikia likiomba misaada badala ya kutumia wafungwa kujenga nyumba zilizobomoka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles