30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wakurugenzi 10 kuhojiwa

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPRA, Balozi Martin Lumbanga
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPRA, Balozi Martin Lumbanga

Na JOSEPH LINO-DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) inatarajia kuwahoji wakurugenzi na wakuu wa taasisi 10 za Serikali kwa kukiuka sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2011.

Hatua hiyo imekuja baada ya ukaguzi wa mwaka 2015/16 uliofanywa na PPRA, kubaini taasisi 10 za Serikali kati ya 70 zilizokaguliwa kuna viashiria vya rushwa, malipo yenye utata na ukiukwaji wa sheria na taratibu za manunuzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPRA, Balozi Martin Lumbanga, alisema wakuu hao wa taasisi wanatarajiwa kuitwa hivi karibuni kuhojiwa ili wajieleze kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu.

Alizitaja taasisi hizo ambazo zimebainika kuwa na mapungufu hayo kuwa ni Taasisi ya Uzalishaji (NIP), Dar es Salaam Rapid Transit (DART), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Makumbusho ya Taifa, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Taasisi ya Mifupa (MOI), Halmashauri ya Manispaa ya Musoma na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Bukoba (BUWASA).

Alisema PPRA inatoa miezi mitatu kwa wakuu wa taasisi zilizofanya malipo yenye utata kurejesha fedha hizo kutoka kwa wakandarasi na kuwasilisha PPRA kwa uthibitisho.

“Ukaguzi wa mwaka 2014/15 ulibaini kuwa taasisi 18 zilifanya malipo ya Sh bilioni 1.32 kwa wakandarasi kwa kazi ambazo hazikufanyika, bodi iliziagiza taasisi hizo kurejesha fedha hizo.

“Lakini katika ukaguzi wa mwaka huu, PPRA imefuatilia utekelezaji wa maagizo hayo na kubaini kuwa taasisi saba ziliyafanyia kazi na kurejesha Sh milioni 370.79, hata hivyo taasisi nane zimekaidi maagizo hayo na kushindwa kurejesha jumla ya Sh milioni 610.07, wakati taasisi tatu zimebaki kimya na kushindwa kurejesha jumla ya Sh milioni 335.22,” alisema.

Pamoja na mambo mengine alisema PPRA itaagiza mamlaka husika kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi waliohusika kwenye miradi 15 iliyopata alama mbaya kwenye ukaguzi wa kupima thamani halisi ya fedha.

Pamoja na hilo alisema PPRA imeshindwa kukagua taasisi zote za Serikali 493 kutokana na ukosefu wa fedha, hivyo iwapo Hazina itatoa fedha za kutosha kwa taasisi hiyo itaendelea kukagua taasisi nyingine hadi kufikia 104 zilizokuwa zimepangwa kwa mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles