MCHEZAJI wa Golf, Rory Macllroy, jana alifanikiwa kuwa bingwa wa michuano ya US PGA Deutsche Bank ya nchini Marekani.
Ushindi wa Macllroy ulifanikiwa baada ya uamuzi wake wa kumwajiri kocha Phil Kenyon, ambaye awali alikuwa akimfundisha Henrik Stenson.
Wakati hivi karibuni kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike ikitangaza kusitisha kudhamini klabu za golf, Macllroy alikuwa chini ya Scotty Cameron kama msaidizi wake.
Akiwa chini ya kocha huyo, hakuonekana akiwa katika kiwango bora michuano ya Bethopage Black yaliyofanyika wiki iliyopita nchini Uingereza kwa Mcllroy kutolewa nje hatua za mwanzoni.
Katika michuano hiyo, alifanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya ushindi alioupata tangu mzunguko wa sita kwa kumshinda Paul Casey, baada ya kupata pointi 65 katika mitupio 6 aliyopata katika mchezo huo uliochezwa uwanja wa TPC Boston, Marekani.
Baada ya kuingia fainali, Macllroy alifanikiwa kushinda mzunguko wa mwisho wa fainali kwa kupiga shuti mbili dhidi ya Casey na kunyakuwa taji hilo kwa mara ya kwanza akifunga.
“Niligundua kitu fulani katika mikono yangu ambayo kwa mwaka huu inanifanya nifanye vizuri,” alisema Macllroy.
Mshindi wa mara nne wa michuano mkubwa ya golf, Casey alishindwa kutamba mbele ya Macllroy.
Ushindi huo kwa Mcllroy una maana kubwa baada ya awali akishuhudia ukienda kwa Jason Day, Jordan Spieth na Dustin Johnson.
Kwani ushindi huo haumfanyi kuwa bingwa wa 12 kufanikiwa katika michuano hiyo, bali utamnyanyua katika viwango vya kimataifa vya golf.
“Kwa kweli safari bado haijafika kikomo kwani ushindi huu ni hatua nyingine ya kufika katika mafanikio wa mchezo huu.
“Nafarijika kuona kiwango changu kikiwa bora, natarajia kuwa zaidi ya hapa nilipo sasa,” alisema Mcllroy.
Kwa sasa McIlroy yupo nafasi ya kufanya vizuri kama alivyofanya katika miaka minne iliyopita.