20.8 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Ndugai ajisikia vibaya Tanzania kukwama Afcon

Job-Ndugai-1Na RACHEL MRISHO, DODOMA

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, ameeleza kuwa amejisikia vibaya sana Tanzania kushindwa kufuzu kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon), zinazotarajia kufanyika mapema mwakani nchini Gabon, wakati Uganda wamefuzu katika fainali hizo.

Uganda ilifikia hatua ya kufuzu baada ya kuichapa Comoro bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mandela, Kampala Uganda na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya watu.

Akizungumza jana Bungeni kwa mara ya kwanza tangu atoke kwenye matibabu nchini India, Ndugai alitoa hisia zake hizo kwa kifupi akieleza kujisikia vibaya.

“Najisikia vibaya Tanzania kushindwa kufuzu Afcon wakati Uganda wenzetu wameweza,” alisema.

Kufuzu kwa Uganda kumewafungua macho Watanzania wengi, ambao nao walitamani Taifa Stars siku moja ingefuzu kwani haijafikia mafanikio hayo kwa muda mrefu.

Uganda imeweza kuvunja mwiko wa miaka 38 na kwenda Gabon, wakati Taifa Stars ikiendelea kusubiri tangu mwaka 1980 ilipokwenda ikiwa chini ya kocha, Joel Bendera na Nahodha, Leodeger Tenga.

Wakati Uganda ikifuzu, Taifa Stars ilitandikwa bao 1-0 na Nigeria katika mchezo wa mwisho wa ratiba ya kukamilisha makundi.

Uganda ni nchi pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), iliyofanikiwa kuingia katika fainali hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles