Na ANDREW MSECHU-DAR ES SALAAM
WASOMI na wachambuzi wa mausala ya siasa wameeleza kuwa mvutano unaoendelea baina ya pande mbili za Chama cha Wananchi (CUF) katika Jimbo la Liwale unaweza kutumiwa kwa faida iwapo viongozi hao watakubali kuwa kitu kimoja kulirejesha jimbo hilo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili jana, wasomi hao walieleza kuwa iwapo viongozi hao – Mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu Maalim Seif wanataka kulirejesha jimbo hilo kupitia kwa mgombea wao Mohamed Mtesa, wanatakiwa kukubaliana kuwa kitu kimoja, la sivyo mgombea huyo atangaze hadharani kuwa yuko upande upi ili atoe nafasi wapigakura kuamua mapema.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Oktoba 13 baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CUF, Zuberi Kuchauka kutangaza kujiuzulu nafasi yake ili kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli, kisha CCM …
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA