Na ASHA BANI
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad amekwenda nchini India kuchunguzwa hali ya afya.
Akizungumza na MTANZANIA jana , Mkurugenzi wa Habari Uenezi Mahusiano na Umma, Salim Biman alisema  Maalim Seif pamoja na kwenda huko hali yake inaendelea vyema.
Alisema siku zote amekuwa akienda kuchekiwa kutokana na utaratibu aliyojiwekea.
“Hizo habari eti anaumwa si za kweli, safari hii ni uchunguzi wa kawaida, hizo zingine ni propaganda tu za mahasimu wetu,’’alisema Bimani.
Katika mitandao mbalimbali ya kijamii, jana zimezagaa taarifa  kuwa maombi yanahitajika kutokana na dharuba kali ya kisiasa  ndani ya CUF jambo lililosababishwa Maalim Seif kukimbizwa India.
Hivi sasa CUF ipo katika mgogoro uliodumu kwa taribani zaidi ya miaka miwili, hali iliyosababisha kuwa mvutano mkubwa wa madaraka.
Hali hiyo, kuwapo na mgawanyiko mkubwa kati ya Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na upande wa Maalim Seif.
Mpaka sasa kuna zaidi ya kesi sita za msingi zimefunguliwa mahakamani.