30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MAALIM SEIF AENDA KUCHUNGUZWA INDIA

Na ASHA BANI

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad amekwenda nchini India kuchunguzwa  hali ya afya.

Akizungumza na MTANZANIA jana , Mkurugenzi wa Habari Uenezi Mahusiano na Umma, Salim Biman alisema  Maalim Seif pamoja na kwenda huko hali yake inaendelea vyema.

Alisema siku zote amekuwa akienda kuchekiwa kutokana na utaratibu aliyojiwekea.

“Hizo habari  eti anaumwa si za kweli, safari hii ni uchunguzi wa kawaida, hizo zingine ni propaganda tu za mahasimu wetu,’’alisema Bimani.

Katika mitandao mbalimbali ya kijamii, jana zimezagaa taarifa  kuwa maombi yanahitajika kutokana na dharuba kali ya kisiasa  ndani ya CUF jambo lililosababishwa Maalim Seif kukimbizwa India.

Hivi sasa CUF ipo katika mgogoro uliodumu kwa taribani  zaidi ya miaka miwili, hali iliyosababisha kuwa mvutano mkubwa wa madaraka.

Hali hiyo, kuwapo na mgawanyiko mkubwa kati ya Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na upande wa Maalim Seif.

Mpaka sasa  kuna zaidi ya kesi sita za msingi zimefunguliwa mahakamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles