29 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

UPELELEZI POLISI WANAOTUHUMIWA KULA RUSHWA WAKAMILIKA

NA FARAJA MASINDE-DARA ES SALAAM

POLISI watatu wanaokabililiwa na mashtaka matano ya kuomba na kupokea rushwa  wanatarajiwa kusomewa maelezo ya awali, Agosti 22, mwaka huu.

Hatua hiyo ilifikiwa Ijumaa iliyopita baada ya upande wa mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuiambia Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika.

Washtakiwa hao  ni Askari PF 20078  Mathias Nkayaga(31) ambaye ni Mkaguzi Msaidizi wa Polisi na mkazi wa Mbezi Mwisho, F 919  D/ Sajenti  Philbert Nemes (39) mkazi wa Kambi ya Polisi Kurasini na  F 3539 Koplo Emmanuel Ndosi ( 37) mkazi wa Survey Mlalakuwa.

Wakili kutoka Takukuru, Devotha Mihayo alisema  upelelezi umekamilika wakati shauri hilo lilipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Ritha Tarimo aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 22, mwaka huu  kwa ajili ya kusomewa hoja za awali kwa washtakiwa hao.

Mihayo  alidai  , washtakiwa kwa pamoja walitenda kosa hilo Februari  27, mwaka huu  katika Kituo cha Polisi  Oysterbay,   Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.

Alidai siku ya tukio, washtakiwa waliomba rushwa ya Sh milioni 25 kutoka kwa mfanyabiashara, Juhudi Kyando kama kishawishi cha kuzuia uchunguzi kuhusu tuhuma za kusafirisha meno ya tembo.

Katika shtaka la pili ilidaiwa katika Kituo cha Mabasi cha Fire (Faya)   Wilaya ya Ilala, washtakiwa walipokea Sh milioni nane kama sehemu ya malipo ya Sh  milioni 25 walizoomba kwa mlalamikaji.

Mihayo alidai katika shtaka la tatu, katika Benki ya CRDB tawi la Lumumba, Dar es Salaam, washtakiwa walijipatia Sh milioni 10  kama sehemu ya malipo ya Sh milioni 25 walizomuomba mlalamikaji,huku shtaka la nne ni kujipatia Sh milioni saba.

Wakili huyo  alidai  katika shtaka la tano, Februari 28, mwaka huu katika eneo la Tabata Bima, washtakiwa hao walijipatia Sh milioni moja kutoka kwa Kyando  kama sehemu ya malipo ya Sh milioni 25 walizoomba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,212FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles