24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

M King Son ‘ambamba’ Tundaman

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kutoka nchini Marekani, msanii wa kizazi kipya mwenye asili ya Kongo, M King Son, ameendelea kupenya kwenye Bongo Fleva baada ya kuachia kolabo yake na staa Tundaman.

Akizungumza na www.mtanzania.co.tz M King Song, amesema wimbo huo unaitwa Amenibamba tayari unafanya vizuri kwenye chati za muziki Afrika Mashariki na kwenye mitandao ya kuuza na kupakua muziki duniani.

“Sina muda mrefu kwenye muziki ila nimepokewa kwa kishindo na mashabiki baada ya kuachia hii ngoma yangu na Tundaman. Huu ni mwanzo wa ujio wa EP yangu ambayo itatoka kabla ya mwaka huu kuisha,” amesema M King Son.

Aidha, mkongomani huyo ametamba kuwa ndani ya EP hiyo kuna kolabo nyingi alizofanya na mastaa wa Afrika Mashariki pamoja na maprodyuza wakubwa lengo likiwa ni kuwapa burudani mashabiki katika ubora mkubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles